ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, January 10, 2013

Ariel Sharon, Waziri Mkuu wa Israel anayeishi kama mfu kwa miaka 7 sasa

 
   
Ariel Sharon akiwa kweny mashine za kumpa uhai kwa miaka  saba sasa
 Ariel Sharon in Coma

 
 
Ariel Sharon akiwa vitani
 
Ariel Sharon enzi za ujana wake


  
Mwaka 1967 Ariel Sharon akiongoza vikosi vya Israel kupambana na Waarabu
   
ariel Sharon Mkuu wa Majeshi wa Israel anayeaminika kuwa katili kuliko wote


 
Sharon akifurahia ushindi wa Israel miaka ya 67


    
Sharon akianza vuguvugu la kisiasa
                                                                             




  
Sharon akiabudu katika Sinagogi kuu Jerusalem

  
Akiwa waziri Mkuu wa Israel mwaka 2001
  
Akifanya amzungumzo ya amani na Bushi huko Camp David

Akiwa na Papa marehemu John Paul wa pili
    
Moja ya ukatili wa Ariel Sharon ambao Wapalestina hawatamsahau na kumpa jina la chinja chinja



Ariel Sharon alikuwa waziri Mkuu wa 11 wa Israel baada ya kulitumikia jeshi kama mwanajeshi matata na mkuu wa majeshi

Sharon alizaliwa 26 february 1928. Alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Israel mwaka 2001 na kazi yake ya uwaziri mkuu iliisha mwaka 2006 aliposhambuliwa na kiharusi/stroke iliyompelekea kulazwa hospitalini katika hali mahututi kuanzia mwaka 2006 hadi leo hii. Amekuwa kwenye hali inayoitwa kwa kitaalamu  "Vegetative state" yaani nusu mfu. Wakati wa uzima wake, Sharoni alikuwa askari machachari mno. Alihisika moja kwa moja katika mauaji ya halaiki ya Qibya mwaka 1953 na Sabra na Shaitila wakati wa vita vya Israel na Lebanon mwaka 1982. Wakati huo  1982 Sharon alikuwa waziri wa ulinzi, alijiuzulu lakini alibaki kama waziri asiyekuwa na wizara maalum. Ni wakati wa utawala wake alitofautiana kisera na wanachama wenzake wa Likud, akaondoka na kuunda chama chake la Kadima.

TArehe 4, Januari 2006, Sharon alipata stroke ugonjwa uliopelekea kukoma kwa utawala wake lakini ugonjwa huu haukukomesha uhai wake.  Sharon ambaye kwa wengi sasa amesahaulika kabisa, bado yuko hai kwa msaada wa mashine. Sharon amekuwa mgonjwa ghali zaidi duniani kwani kwa mwezi analipiwa uro 300,000 ambazo nusu zinatolewa na familia yake na nnusu zinatolewa na Serikali ya Israel.

Kwa uamuzi wa familia yake, yaani watoto wake wawili  Gilad na Omri Sharon waliamua kuendelea kumtunza na hivyo kuwa mgonjwa wa kwanza duniani kukaa katika hali ya umahututi kwa muda mrefu. Kwa kuwa Sharon na familia yake hawakuwa watu wa kushika dini, haijulikani ni lini wataamua kuzima mashine zinazoendelea kumpa uhai. Msemaji wa Hospitali ya Sheba ambako Ariel Sharon amelazwa katika chumba cha peke yake alipoulizwa kuhusu hali yake alisema kwamba Sharon ambaye sasa ana miaka 83, yuko fiti katika hali isiyobadilika na isiyotarajiwa kubadilika. Hakuna mwanasiasa au daktrari yeyote anayeruhusiwa kuongea chochote kuhusu afya ya waziri huyo wa zamani wa Israel. 
Je wewe na mimi tunaweza kusema Sharon amekufa, au yu hai? au ni vyote viwili?



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...