ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, January 10, 2013

Wamiliki Vyombo vya Habari, Wahariri na Baraza la Habari Watoa Maoni Katiba Mpya Leo



Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT) Bw. Reginald Mengi akitoa maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Alhamisi, Jan 10, 2013) katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Tume hiyo Prof. Palamagamba Kabudi.
Mwanachama wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Deodatus Balile akiwasilisha maoni ya Jukwaa hilo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo  (Alhamisi, Jan 10, 2013). Wengine ni Bw. Ruge Mutahaba (kushoto) kutoka Clouds Media Group na Bw. Yasin Sadik kutoka gazeti la Hoja. 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bw. Kajubi Mukajanga akiwasilisha maoni ya Baraza hilo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo  (Alhamisi, Jan 10, 2013). Kulia ni Bi. Pili Mtambalike kutoka MCT.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Absolom Kibanda akimkabidhi maoni ya Jukwaa hilo kuhusu katiba Mpya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo  (Alhamisi, Jan 10, 2013).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...