Jukwaa
la kiuchumi duniani limefunguliwa rasmi mjini Davos nchini Uswisi hii
leo ambako takriban viongozi 45 duniani pamoja na wanaharakati 2500,
waandishi habari, wakuu wa kibiashara na wanauchumi wanahudhuria.
Mkutano
huo wa kila mwaka ambao unafanyika kwa siku tano umeanza kwa kujitokeza
hisia za kuwepo matumaini kwamba hali mbaya ya kiuchumi huenda ikawa
imefikia mwisho.
Tofauti
na ilivyokuwa katika mkutano wa mwaka jana, ambapo ulitawaliwa na mzozo
wa kiuchumi barani Ulaya pamoja na hofu kwamba Ugiriki huenda
ikatimuliwa katika kanda ya Euro.
Katika
ufunguzi muasisi wa jukwaa hilo na muandaaji Klaus Schwab mwenye umri
wa miaka 74, ametoa wito kwa wajumbe kulishughulikia suala la mgogoro wa
madeni katika kanda ya Euro, ambao umelisogeza eneo hilo katika
mporomoko wa kiuchumi.
No comments:
Post a Comment