Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Ernest
Brandts amesema timu yake itafanya vizuri katika mechi ya marudiano ya
kirafiki dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini niliyopangwa kufanyika
mapema jioni ya leo ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba mjini Mwanza.
Brandts alisema wachezaji wake wote
wamefikia kiwango kile anachotaka na mchezo huo utakuwa muhimu sana
kwake kwani ni wa mwisho kabla ya kuingia katika kampeni za kutwaa
ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Alisema kuwa Black Leopards ni timu
nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza iliyofanyika
kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.
“Ni mechi nzuri ambayo nadhani itakuwa
ni kipimo kikubwa kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara,
wachezaji wangu wana viwango vizuri sana kwa sasa na naamini makosa
yaliyofanyika katika mechi ya kwanza hawatayafanya tena,” alisema
Brandts.
Msemaji wa Klabu Yanga, Baraka Kizuguto
alisema jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya maandalizi ya Ligi Kuu ya
Tanzania Bara, pia wameamua kuicheza ili kuwapa burudani mashabiki wa
Mwanza.
Kizuguto alisema kuwa Yanga haitakuwa na
mechi yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya ziwa na hiyo ndiyo nafasi
yao ya kuwaonesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa Mwanza nini wamekipata
kutoka Uturuki.
“Tuna mashabiki wengi sana Mwanza na
Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu kwani mahsbaiki na
wanachama watapata fursa ya kuona kiwango na maandalizi ya timu yao
kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili,” alisema Kizuguto.
No comments:
Post a Comment