ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, January 5, 2013

Kiongozi wa Waasi “M23” (Askofu Jean Marie Runiga azungumzia wanyonge wanavyotaabika Congo .


 
 
  

 
  
  
 
 
  
 
 

 


Kiongozi wa kundi la uasi la M23, Jean Marie Runiga amezungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika Ijumaa katika mahojiano ya moja kwa moja na kusema yeye ni mtumishi wa Mungu na kwamba  ni askofu aliyeamua kuunda kundi la waasi  ili ‘kutetea haki za wanyonge’  katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
Bw. Runiga amesema  Mungu hapendi kuona binadamu wakitaabika  na hivyo aliona  kheri kuanza juhudi  kuwakomboa wakongomani ambao hawajui maisha mengine ila taabu na mateso. Kiongozi huyo wa M23 amesema serikali ya Kabila imeshindwa kuwahudumia raia wa Congo na kwamba wengi wanakufa kila siku sio kwa sababu ya vita bali ukosefu wa huduma za kimsingi kama vile chakula na matibabu.
 
Alisema  DRC haina miundombinu, haina barabara, haina hospitali , wala shule za kutegemewa. Alisema wanawake wanazidi kubakwa yote haya akilaumu uongozi anaosema si halali wa serikali ya Rais Joseph Kabila. Bw. Runiga amesema mwishoni mwa wiki hii kundi lake na wawakilishi wa serikali ya DRC wanakutana Kampala, Uganda kuendela na juhudi mazungumzo ya kutafuta amani nchini Congo. Alisisitiza kuwa kundi lake linatoa nafasi ya amani kwanza, kwa ajili ya raia wa Congo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...