ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, January 5, 2013

WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe:“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge

WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe 
----
WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.

Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.

“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,” alisema Membe.

Ambapo pia aliwataka wananchi wa mikoa ya kusini, kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo Serikali inashughulikia mchakato wa kuvuna gesi asilia.Alisema kuwa ni muhimu kwa wakazi wa mikoa iliyopatikana gesi kutambua kuwa rasilimali zinazopatikana nchini ni mali ya Watanzania wote na siyo ya mikoa iliyogundulika pekee.

Waziri Membe aliwataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, kuacha kutumia vikao vya halmashauri kujadili malumbano yasiyokuwa na msingi akisema kwamba kufanya hivyo ni kupoteza rasilimali za wananchi bila faida.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...