MAKAMU
wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilali anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maulidi ya
kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Mohamed (SWA), yatakayofanyika katika
viwanja vya Mnazimoja, jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza jijini jana,
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salim, alisema siku hiyo ni muhimu
kwa waumini wa dini ya kiislam wote dunia ambapo yatanza saa 3:00 usiku katika
viwanja hivyo.
Alisema waislam wote
wajitokeze kwa ajli ya kwa ajili ya kumbukumbu hiyo, ambapo ujumbe wa safari hii
ni ‘Tudumishe amani na utii wa sharia kwa wote’.
Aidha, sherehe hizo ni za
kidini hivyo, ni lazima kila atayehudhuria katika viwanja hivyo asitoke nje ya
mipaka ya dini, na atakayekwenda kinyume atakuwa amejitafutia laana kutoka kwa
Mnyazi Mungu.
No comments:
Post a Comment