
Mtuhumiwa
wa nyara za serekali Peter Laurence (mwenye kofia katikati) akiwa na
maofisa wa jeshi la polisi chini ya ulinzi ,eneo la Kisongo mtaa wa Mateves nje kidogo ya jiji la Arusha baada ya kukamatwa na shehena ya nyara za serikali nyumbani kwake.
Miongoni
mwa nyara za serekali zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu
nyumbani kwa mtuhumiwa Peter Lawrence zikionekana kwenye maboksi
tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.
Maofisa
wa jeshi la polisi wakitoa mabox yenye nyara za serekali kwenye ghala
la mtuhumiwa teyari kwa kuzisafirisha kwenda kwenye kituo kikuu cha
polisi jijini Arusha.
Pichani
ni ngozi ya Mamba ambayo ilikutwa kwenye ghala la mtuhumiwa ikiwa ni
sehemu ya nyara mbali mbali zilizokutwa kwenye ghala hilo ikiwemo meno
ya tembo, vichwa vya simba,vichwa vya nyati, ngozi ya simba, ngozi ya
tembo na nyara nyingine nyingi za wanyama mbali mbali.(picha zote na
Mahmoud Ahmad-Arusha).
Mahmoud Ahmad Arusha
Jeshi
la polisi mkoani Arusha, limekamata shehena kubwa ya nyara mbalimbali
za serikali zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu,eneo la
Matevesi Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha zikiwa tayari kwa
kusafirishwa nje ya nchi.
Nyara
hizo ni pamoja na Ngozi za Simba,Chui na Mamba ,meno ya Tembo,vichwa
vya Nyani,Swala na Nyati, Pembe za kifaru,na zingine nyingi ambazo jeshi
la polisi linaendelea kuzitambua.
Sambamba
na hilo jeshi hilo limemtia mbaroni mtuhumiwa wa nyara hizo
aliyetambulika kwa jina la Peter Leurence (55)mkazi Ngaramtoni ya
chini,ambaye alikuwa akiwa amezihifadhi kwenye maboksi zaidi ya
20,kwenye nyumba yake iliyopo eneo hilo.
Kwa
mujibu wa kamanda wa polisi mkoni Arusha,Liberatus Sabas tukio la
kukamatwa kwa nyara hizo limetokea jana majira ya saa 6.30 usiku wa
kuamkia leo eneo la Kisongo mtaa wa Mateves baada ya kupata taarifa
kutoka kwa raia wema.
Kamanda
Sabas alisema kuwa baada ya jeshi hilo kupata taarifa za siri majira ya
saa 5 asubuhi walifika eneo la tukio majira ya saa 7 mchana na kupata
upinzani mkubwa kutoka kwa walinzi wa wanaolinda eneo hilo kwani
waliwanyima kuwapa maelekezo ya kumpata mmiliki wa nyumba hiyo.
Hata
hivyo alisema kwamba askari hao waliamua kumueka chini ya ulinzi kwa
kumshurutisha mlinzi mmoja iliaweze kuwapa ushirikiano ambapo aliwapaita
namba za simu na mtuhumiwa aliwaambia kuwa yupo magugu mkoani Manyara
na angefika saa 12 majira ya jioni.
Taarifa
zinadai kuwa baada ya mtuhumiwa kufika jitihada za kufanya upekuzi
zilifanyika chini ya polisi wenye silaha za moto na walikuta shehena
kubwa ya nyara za serekali zilizokuwa zimahifadhiwa kwenye ghala maalum
na kufungwa kwenye mabox teyari kusafirishwa kwenda kusikojulikana.
Alisema
kuwa polisi waliamua kuweka ulinzi hadi kulipokucha na huku wakiendelea
kumshikilia mtuhumiwa huyo na jeshi hilo linaendelea kumshikilia
mtuhumiwa huyo pamoja na watoto wake wawili waliokutwa wakiishi kwenye
nyumba hiyo.
Aidha
kamanda Sabas alisema kuwa kesho yake polisi waliendelea kufanya
upekuzi na kubaini mabox zaidi ya 20 yenye nyara mbali mbali miongoni
mwa nyara hizo alizitaja kuwa ni Ngozi za Chui.Simba,Tembo na Mamba pia
kulikuwemo vichwa vya nyani,chui,swala nyati,pembe za faru , meno ya
tembo na nyingine nyingi ikiwemo mfuko wa silaha inayosadikiwa
kuhifadhia silaha.
Kwa
mujibu wa kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa alisema kuwa
Watuhumiwa bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano na
watafikishwa kwenye mahakama pindi upelelezi wa tukio hilo utakapo
kamilika.




No comments:
Post a Comment