
Pichani
Juu na Chini ni Wananchi wakivuta katika sehemu itayojengwa darala la
kisasa la Mbutu la Igunga ambao ujenzi wake umezinduliwa leo na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, hatua ambayo itatatua kabisa tatizo la
miundombinu.


Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia mashine ya kuchimbia mashimo ya nguzo
za daraja na baadaye anakata utepe kuzindua ujenzi daraja la Mbutu la
Igunga.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mawaziri, wabunge na maofisa waandamizi
wa wizara na wakala wa ujenzi (TANRODS) pamoja na viongozi wa bodi ya
wakandarasi akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa daraja hilo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mradi wa Chujio la maji safi kwa mji wa
Igunga sehemu za Bulenya ambapo wakazi asilimia 70 wa mji huo watapata
maji safi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tanroads,Eng. Patrick Mfugale (alieshika maiki) akumuonyesha
Rais Kikwete ramani ya Mradi wa Ujenzi wa daraja la kisasa katika eneo
la Mbutu,Wilayani Igunga.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakipozi na umoja wa
wakandarasi wazalendo kutoka makampuni mbalimbali waliopewa kandarasi ya
kujenga daraja hilo.(PICHA NA IKULU).

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na kutoa ushauri kwa kundi la vijana 10
ambao baada ya kumaliza chuo kikuu wamejikusanya na kuunda kikundi cha
ujasiriamali mjini Igunga wakijishugulisha na Kilimo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amesema kuwa Serikali yake inakaribia kukamilisha ujenzi wa madaraja
yote 10 yaliyoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na
ambayo yanagharimu mabilioni ya fedha.
Rais
Kikwete amesema kuwa kati ya madaraja hayo ambayo thamani yake
inakaribia sh. bilioni 415, madaraja mawili tayari ujenzi wake
umekamilika. Madaraja hayo ni lile la Ruhekei lililoko Wilaya ya Mbinga
katika Mkoa wa Ruvuma na Daraja la Mwatisi katika Mkoa wa Morogoro.
Rais
Kikwete amesema kuwa madaraja mengine saba yanaendelea kujengwa, ikiwa
ni pamoja na Daraja la Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam linalogharimu
sh bilioni 214.6, Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi, Mkoa wa
Kigoma unaogharimu sh bilioni 90.185, Daraja la Kilombero, Mkoa wa
Morogoro linalogharimu sh bilioni 53.214 na Daraja la Rusumo, Mkoa wa
Kagera linalogharimu sh bilioni 31.7.
Madaraja
mengine yanayoendelea kujengwa ni Daraja la Sibiti, Singida,
linalogharimu sh bilioni 17.5, Daraja la Nangoo, Mkoa wa Mtwara
linalogharimu sh bilioni 4.29 na Daraja la Maligisu, Mwanza,
linalogharimu sh bilioni 2.51.
Amesema
Rais Kikwete: “Madaraja niliyotaja ujenzi wake ukikamilika, tutakuwa
tumetimiza ahadi yetu ya kujenga madaraja yote yaliyotajwa katika Ilani
ya Uchaguzi ya mwaka 2010 isipokuwa Daraja la Ruhuhu ambalo maandalizi
yake ya ujenzi yanaendelea.”
Rais
Kikwete alikuwa anazungumza wakati anaweka jiwe la msingi kwa ajili ya
ujenzi wa Daraja la Mbutu, Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora katika
sherehe ya kufanya iliyofanyika Jumatatu, Januari 7, 2013.
Rais
Kikwete amesema kuwa baadhi ya madaraja yanayojengwa sasa na Serikali
yalipangwa kujengwa katika Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo mwaka
1968 lakini kwa bahati mabaya hayakuweza kujengwa. Madaraja hayo ni
Daraja la Kigamboni, Daraja la Kirumi kwenye Mto Mara, Daraja la Rufiji,
Daraja la Kilombero, Mkoa wa Morogoro na Daraja la Kikwete kwenye Mto
Malagarasi.
Awamu
ya kwanza ya uongozi wa nchi yetu ilijenga Daraja la Kirumi kwenye Mto
Mara, Awamu na pili ikafanya maandalizi na Awamu ya tatu ikajenga Daraja
la Rufiji na Awamu ya sasa inajega madaraja matatu yaliyobakia –
Kilombero, Kigamboni na Kikwete.”
Daraja
la Mbutu lina urefu wa kilomita tatu, na linajengwa katika Bonde la
Mbutu na litaunganisha mikoa ya Tabora, Singida, Simiyu na Shinyanga.
Daraja
hilo litakuwa na daraja moja kubwa la mita 60 na madaraja mengine
madogo saba na hivyo kufanya urefu wa daraja lote kuwa na mita 165.
Mpaka sasa asilimia 45 ya ujenzi wa daraja hili lenye thamani ya sh
bilioni 11.28 umekamilika na inakadiriwa kuwa litakuwa tayari ifikapo
Novemba mwaka huu.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
7 Januari, 2013






No comments:
Post a Comment