ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, January 17, 2013

MKE WA RAIS NA MWENYEKITI WA TAASISI YA WAMA AFUNGA MKUTANO WA MAMA NA MTOTO LEO JAN 17,2013-ARUSHA



1- Mama Jk (kushoto) akielekea ARS ((kushoto) NW wa Afya Dr. Seif Rashid
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete(kushoto) pamoja na Naibu wa Wizara ya Afya Dkt.Seif Rashid (mwenye miwani) wakielekea kupanda ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa- JK- Nyerere jijini Dar es Salaam 16-jan 2013 kuelekea Arusha kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya na Mtoto jan. 17,2013. Mkutano huo unawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi. (picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
2- MMama Salma akisalimiana na wafanyakazi wa ndege- (kulia) NW wa Afya Dr. Seif Rashid
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akisalimiana na wafanyakazi wa ndani ya ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam Jan 16,2013 wakati akielekea kufunga mkutano wa Masuala ya Afya na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Mkutano huo anawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi, (kulia) ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
3-- Mama Jk akiangalia ngoma ya utamaduni wakati wa mapakeezi, (mwenye miwani) ni Mk wa uwt -kILIMANJARO MAMA  FLORA ZELOTE
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete(kulia) akiangalia vikundi vya sanaa ya ngoma mbalimbali za utamaduni alipowasili katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimnjaro (KIA) jan 16.2013 kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya ya Mama na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Aliengozana nae wapili ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Arusha (UWT) Flora Zelote (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
4-KIKUNDI CHA NGOMA YA MSANJA KIKITUMBUIZA
Kikundi cha kinamama cha ngoma ya Msanja kikitumbuiza katika mapokezi ya Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama salma Kikwete (hayupo pichani) kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA ) Jan 16,2013.(Picha na Mwanakombo Jumaa wa MAELEZO).
7-MAMA JK (KULIA) AKISALIMIANA NA MKUU WA MKOA WA ARSMwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Wanawake(WAMA) kulia, Mama Salma Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa Arusha Magesa Mulongo (kushoto) wakati alipowasil katika Uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA) Jan 16,2013.- Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
8- Mama jk (kulia) akisalimiana na mkuu wa wilaya ya ars John Mongela- KIa
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Jan 16,2013. –Picha na Mwnakombo Jumaa- MAELEZO.
………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
Kauli mbiu ya kongamano la ulimwengu la Afya ya uzazi linaloendelea jijini Arusha imepewa msisitizo na kuwa hakuna mama atakayekufa wakati akileta kiumbe duniani na pia Afya ya mama na mtoto ipewe kipaumbele.
Kauli hiyo imeendelea kutolewa na Mke wa Rais mama Salma Kikwete wakati akiwasilisha na kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo jijini hapa na kuwataka watafiti na wataalamu hao kuja na majibu yatakayosaidia kupunguza vifo vya wakinamama wakati wa kujifungua.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...