ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, January 12, 2013

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema Amkabidhi pikipiki 546 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza


 Afande Inspekta Mkweru akijaribu moja ya pikipiki zilizokabidhiwa leo kwa maafisa wa jeshi hilo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova kama ishara ya kukabidhiwa Makamanda wote Tanzania bara na Visiwani ambapo jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza.Makabidhiano hayo yamefanyika katika makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Makamanda na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kovaakijaribhu mkuwasha moja ya pikipiki zilizotolewa kwa maofisa mbalimbali wa jeshi hilo nch nzima mara baada ya makabidhiano anayeangalia katikati na Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema na kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi Kikosi cha Mbwa na Farasi Tanzania Mrakibu wa Polisi Eugen Emmanuel, kwa ajili ya matumizi ya Programu ya Usalama wetu Kwanza.jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza.
 Baadhi ya Wakaguzi wa Tarafa wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wakiwa katika pikipiki zao baada ya kukabidhiwa katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, ambapo jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza
 Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa maafisa hao wa polisi leo
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema kulia akiwa katika hafla ya makabidhiano hayo makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es salaam leo asubuhi, katikati ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonjaakizungumza jambo na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania Advera Senso wakati wa hafla hiyo.Picha na Mroki Mroki

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...