ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, January 10, 2013

Msako mkali unaoendelea Kenya wapelekea Majangili wawili kuuwawa na mmoja raia wa Congo akamatwa

 
 
ISIOLO, Kenya; Polisi wa Kenya pamoja na idara ya wanyamapori wamesema kwamba wamewauwa raia wawili kwa kuwapiga risasi baada ya majibizano ya risasi. Majangili hayo yalikuwa yameuwa Tembo wanne katika  mbuga ya Isiolo. 
Uwindaji haramu wa Tembo ulipungua baada ya mwaka 1989 wakati Serikali ya Kenya ilipopiga marufuku uwindaji wa Tembo. Lakini uwindaji haramu umeanza tena kwa wingi siku za hivi karibuni baada ya bidhaa hizo kuhitajika sana katika bara ya Asia hususan  Uchina. 
Polisi wa Kenya pamoja na askari wa wanyamapori wa Kenya (KWS) wamesema kabla majangili hayo hayajauwawa, kulikuwa na majibizano ya risasi kati yao na majangili hayo juzi katika mbuga ya Idiolo. Majangili wawili waliuwawa na silaha mbali mbali walizokuwa wanatumia ziilikamatwa,
Hata hivyo, msemaji wa KWS ameseka kuwa, Jumapili iliyopita walikamata maharamia wawili Isiolo wakiwa tayari na meno ya tembo  na.silaha.
Mwishoni mwa wili iliyopita, kundi kubwa la maharamia lilivamia familia moja ya tembo na kuwauwa wote kumi na moja na ndama mmoja. Huu  ni uuwaji wa kutisha na wa kihistoria katika historia ya kenya. Kenya inasadikiwa kuwa na tembo  39,000 kwa sasa.  Waziri Mkuu Raila Odiga alisema jana kwamba mwaka jana pekeee tembo 360 waliuwawa wakati mwaka juzi (2011) tembo 289 waliuwawa. Hivyo hatari ya kutoweka kabisa kwa wanyama hao inazidi kuwa kubwa kila siku.
Uchumi wa Kenya unategemea kwa kiasi kikuutalii hivyoo daji haramu wa wanyama hao unaendelea kuhatarisha kutoweka kwao na hivyo uchumi wa Kenya kuyumba kabisa.
 
  
Polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akiwa ameshikilia meno ya tembo. Katika tukio hilo, watu wawili raia wa Kenya na mmoja Mtanzania, walikamatwa maeneo ya Kimara stopover wakiwa na meno 214 ya tembo pamoja na mofupa mingine ya wanyama yenye thamani ya singi bilioni 2.1 
 
Tanzania nayo inakabiliwa na changamotokubwa pengine zaidi kuliko Kenya kutokana na kutokupatikana mara kwa mara kwa taarifa za uharamia huu. Inakadiriwa kuwa kwa TanzaniaTembo 30 wanauwawa kila siku (http://www.elephant-news.com/index.php?country=Tanzania) ambapo kwa mwaka wanauwawa tembo takriban 10,000. Idadi ya tembo waliopo Tanzania kwa sasa wanakadiriwa kuwa 150,000. Kw abara zima la Afrika mwaka 1977 kulikuwa na Tembo 1,300,000 ambapo kwa saa tembo kwa bara zima wamebakiwa 470,000 tu. Ukweli ni kwamba, biashara hii ni tamu sana na ina pesa nyingi sana. Ni kishawishi kikubwa kwa wananchi na hata viongozi wasio waaminifu kujihusisha nayo. Haiingii akilini mzigo unanaswa Sri lanka ukiwa umeshapita bandari zote na umepatiwa vibali vyote, kama sio mikono ya wakubwa ni nani? Baadhi ya viongozi wetu na wale wote wanaojihusisha na biashara hii wana roho ya kutaka kupata vyote leo. Wanajiona kuwa wao ndiyo wenye haki ya kufaidi sasa na vizazivijavyo havina haki hiyo. Wana uchoyo na uroho wa mali kiasi ambacho hata hawawezi kukitumia. Filosofia ya Afika ni uchoyo, tena uchoyo ambao "sio tu ni kiasi gani mimi ninapata, lakini pia ninahakikishaje mwengine hawapati kabisa?" Huu ni zaidi ya uchoyo, ni zaidi ya roho mbaya, ni zaidi ya dhambi. Hivyo suala la uwindaji haramu litabaki kudelea kuwa wimbo tu mpaka uwepo wa tembo na wanyama wengine utakapobaki kuwa historia.



(Organised poaching, illegal trade - why Tanzania lost out at Cites meet

2010-03-28 - Addis Abeba, Tanzania
A new investigation by a panel of international and local experts that implicated senior government officials in the illegal ivory trade and the rise in elephant poaching in Tanzania is believed to have led to the country being denied permission for a one-off sale of its $20 million ivory stockpile.)
http://www.elephant-news.com/index.php?country=Tanzania 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...