ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, January 16, 2013

SAKATA LA KUBOMOLEWA NYUMBA NA MGAHAWA MTAA WA OHIO JIJINI DAR ES SALAAM


 Rubani Mstaafu wa Ndege za Serikali, Felix Henry Kileo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya tukio la kuvinjiwa nyumba namba 15 aliyokuwa akiishi na kufanya biashara katika kitalu namba 223/50 kilichopo mtaa wa Ohio jijini humo. Kwa Mujibu Wa wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) Kiwanja hicho kinamilikiwa na Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) na Benki hiyo inataraji kujenga Makao makuu ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). 
Rubani huyu alidai kitendo cha kubomolewa nyumba yake ni cha kinyama kwani yeye alikuwa mtumishi wa serikali kama rubani na katika kipindi chote cha utumishi wake hakuwahi hata siku moja kupata ajali hata pancha akiendesha Viongozi kama Marais.
 Kutokana na kuta za nyumba hiyo kuwa ngumu kazi ya ubomoaji ililazimika kuanzia madirishani ili kurahisisha ubomoaji.
 Vitu vikiwa nje
Vyombo vilivyokuwa vikitumika upande wa Biashara vikiwa nje.Mgahawa ulikuwa maarufu kama Kwa Mama.Picha na Habari na Mdau Mroki Mroki

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...