Zitto Kabwe
ASILIASerikali iache kutafuta
mchawi, iende Mtwara
Katika
kipindi cha wiki nne sasa kumekuwa na maandamamo, malumbano na vurugukuhusu
mradi wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar
esSalaam. Mradi huu wa kutandaza bomba la urefu wa kilometa 542 ni mkubwa
sanahapa nchini, na una thamani kubwa zaidi kuliko miradi mingine yote ya
miundombinuiliyopata kutokea hapa nchini.
Mradi huu utajengwa kwa mkopo wa dola zaKimarekani 1.2 bilioni kutoka
Benki ya Exim ya China.Wananchi wa Mtwara kupitia maandamano ya tarehe 27
Desemba 2012 wametakakujua hatma ya maendeleo ya mikoa wa kusini kutokana na
mradi huu wa bomba lagesi. Serikali
imewajibu wananchi hawa kwa kuwaita wahaini, watu hatari na wasioelewa.
Imefika mahali inapotosha madai yao kwamba hawataki gesi itoke Mtwara.Kimsingi Serikali haijajibu hoja yeyote ya msingi
ya wananchi wa Mtwara kuhusumradi wa kusafirisha gesi. Badala yake
imekuwa ikijaribu kupotosha madai ya watuwa Mtwara kupitia mikutano na vyombo
vya habari.Tangu maandamano haya yatokee, na
baadaye mikutano ya hadhara nahatimaye
matukio ya kusikitisha ya kuharibu mali za watu, mauaji yawatu na majeruhi mbalimbli, Serikali na hasa Wizara
yenye dhamana yamradi huu, imekuwa ikitoa matamko kwenye vyombo vya habari
badala yakwenda Mtwara kuzungumza na wananchi, kusikiliza madai yao na kuonanamna
ya kutekeleza madai hayo. Kutokana na Serikali kutofanya hivyo,kusikiliza
na kuzungumza na wananchi wa Mtwara, vurugu mbaya sana zimeendeleamkoani humo.Mwezi uliopita, Desemba 2012, tatizo lilionekana
kuwa ndogo na lenye kuhusianazaidi
na ukosefu wa kushirikishwa kwa wananchi. Badala ya kushughulikiatatizo likiwa bado ndogo, Serikali imeona njia
pekee ya kushughulikia suala hili nikutafuta
mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisemakuwa w
anasiasa namakampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogorohuu
.Leo hali iliyopo mkoani Mtwara inasikitisha sana,
maana mali za wananchizinaharibiwa,
nyumba zinachomwa moto na watu wanapoteza maisha. Tunalaanimatukio haya kwa nguvu zetu zote, maana kinachotokea
Mtwara si Utanzania.Tusipowasikiliza wananchi na kutatua mgogoro huu kwa
kuwashirikisha, hali itazidikuzorota wakati tukitupiana lawama.Hivi sasa
serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi nakwa
wiki zote hizi
imekuwa
ikisema kuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezajiya nje yanachochea mgogoro huu
.Kwanza, Serikali imekuwa ikiaminisha umma kwanza
suala hili limechukuliwakisiasa. Pili, Serikali imekuwa ikirudia kusema kuwa baadhi
ya makampuni ya
uwekezaji nchini na mataifa ya Magharibi yamekuwa
yakichochea wananchi waMtwara.Katika
mwendelezo wa mtindo wa Serikali wa ‘
management
by press conferences’
jana
Jumamosi Naibu Waziri wa Nishati na Madini ndugu George Simbachawenealiwaambia wahariri kwamba mimi Zitto Kabwe
ninachochea wananchi wa Mtwara,ninatumiwa, na si mzalendo. Vile vile
alitoa vielelezo kadhaa kuonyesha kuwa mradiwa
kujenga bomba la gesi ni gharama sawasawa. Akasisitiza kwamba mimi nimwongo.Katika kipindi chote cha mgogoro wa Gesi Mtwara,
sijafika Mtwara. Sijafanyamkutano
wowote na waandishi zaidi ya kuandika mawazo yangu, kama Mtanzaniakuhusu
suala hili.Nimeandika makala nne na zimechapishwa katika magazeti kadhaa hapa
nchini nakwenye blogu yangu (http://zittokabwe.wordpress.com/).
Niliandika:
Nikaandika tena:Mtwara:Serikali inavunja nchi kwa kutosikiliza Wananchi ;
ni baadhi ya makala nilizoandika kuhusiana na
suala la Mtwara. Sitaki kubishana na
Naibu Waziri ama Kiongozi yeyote ya Serikali kwa sasa.Hatuwezi kuendelea kulumbana, kuzozana, kuzodoana
na kurushiana manenowakati nchi yetu
inaungua. Huu sio wakati wa kutafuta mchawi bali kutafutamajawabu ya
changamoto zilizopo mbele yetu.Yanayotokea Mtwara ni fundisho kwetu kwa Taifa
namna ya kukabili changamoto zautajiri wa rasilimali, ili kuweka mkakati, mambo
haya yanayotokea Mtwara yasitokeetena Tanzania. Tutaweza kuzuia maafa haya
iwapo tutaweka uwazi katika mikataba,tutashirikisha
wananchi kwenye unyonyaji wa maliasili za nchi, na iwapo tutawekauwajibikaji.
Rais
Kikwete Kikwete ana majibu; ayatoe sasa kwa wana Mtwara
Kwa mujibu wa Mpango Kabambe wa Umeme nchini (Power
System Master Plan),kulikuwa
na mradi wa kufua umeme MnaziBay, ambao Rais Jakaya Kikwete aliagizautekelezwe
mara moja. Serikali ieleze umma kuhusu mradi huo wa kujenga kituo chakufua
umeme 300MW MnaziBay Mtwara na kujenga msongo wa umeme wa 300KVmpaka Singida. Umeishia wapi? Ikumbukwe kuwa mnamo
tarehe 12 Oktoba 2012,Rais Jakaya Kikwete alipokea ripoti ya ujenzi wa mradi
huu kutoka makampuni yaChina National Machinery & Equipment Import &
Export Corporation (CMEC) yaChina na
Siemens ya Ujerumani, ambayo kwa pamoja yalitarajia kujenga kituokikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi
katika eneo la Mnazi Bay, mjiniMtwara na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme
ya kilomita 1,100 kutoka Mtwarahadi Singida. Mradi huu ungegarimu dola
za kimarekani milioni 684 na Rais aliagizautekelezwe
haraka sana. Huu mradi uliishia wapi? Kwa nini Serikali ipo kimya
kuhusu mradi huu ambao ungejibu kabisa maswali ya watu wa
Mtwara?
Taarifa
yaIkulu kuhusu mradi huu imeambatanishwa hapa Tufanyeje?
Hapa tulipofikia ni lazima kwanza kabisa kusikia kilio
cha wananchi wa Mtwaraikiwemo
kuelewa madai yao. Swali kubwa kubwa la watu wa Mtwara na Kusini kwaujumla ni ‘tunanufaikaje’? Jibu la swali hili si
ahadi za miradi bali ni vitendo. Hapandipo serikali inaposhindwa
kushughulikia suala hili, kutoelewa madai ya wananchina kuyapotosha.Viongozi wa kisiasa wenye ushawishi kutoka pande zote,
chamatawala na vyama vya upinzani, waende Mtwara kuzungumza na wananchi, lakiniwawasikilize
kwanza.
1.Lazima
viongozi tujenge utamaduni wa kusikiliza wananchi na si kuwahutubia tu. Wananchi wa Mtwara wana madai ambayo lazima
viongozi tukae kitakokuwasikiliza kisha kufanya nao majadiliano ambayo yatatoa
mwafaka. Raismstaafu,
Ndugu Benjamin Mkapa ameshatoa kauli kuhusu suala hili.
Ni wakati mwafaka
sasa kwa viogozi wengine kumuunga mkono kwakwenda Mtwara na kukaa na wananchi
wa Wilaya zote za Mtwara,kusikiliza hoja zao na kuona namna ya kupata ufumbuzi wa
suala hili.Wakati hatua hii inachukuliwa, wananchi waombwe kutulia na kuachavurugu za aina
yeyote ile, na Serikali isimamishe mradi mpaka haposuluhu na wananchi itakapopatikana
.
2.Wakati
juhudi hizo zinaendelea
Serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi wabomba, kwani ni dhahiri gharama za
mradi huu ni kubwa mno kulinganana uhalisia wa miradi ya namna hii duniani
kote. Katika taarifa zote kwaumma Serikali
imekuwa ikisema kwamba mradi utagharimu jumla yadola za kimarekani 1.2 bilioni,
lakini katika taarifa ambayo Wizara yaNishati na Madini imesambaza jana
kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini
imesema mradi utagharimu dola za kimarekani milioni 875. Usiri katika mkataba
huu unaashiria kwamba Serikali inaficha kitu.
Hivyo njiapekee ni kutaka mkataba uwe wazi kwa wananchi.
3.Wakati tunawataka wananchi wa Mtwara kuruhusu
utulivu, ni vema Serikali ijiandae kutoa majawabu ya madai ya wananchi
hao. Majawabu ya Serikali yajikite kueleza wananchi wa Mtwara
wanafaidikaje na rasilimali ya gesi asiliakwa
maendeleo yao. Wananchi wa Mtwara wanataka uwajibikaji wa Serikali kwenye utajiri wa nchi, na wamechoka na porojo za
orodha ya miradi isiyotekelezwa
.Viongozi twendeni Mtwara kusikiliza wananchi wetu.
Nchi inaungua na hatuwezi kuendelea kuzozana badala ya kuzima moto huu
hatari kama vita vya MajiMaji. Miminakwenda
Mtwara haraka na mara baada ya viongozi wangu wa chama kutoa ridhaa.
ZITTO KABWE
Mbunge, Kigoma Mjini (Chadema)Waziri
Kivuli wa Fedha
No comments:
Post a Comment