Uongozi wa TRA Kinondoni Tawi la M
wenge ukiongozwa na mrs rehema Shao (Makamu Kamishna wa TRA Kinondoni)Mariam Mwamile, Emmanuel Mahendelu, Evarist Munishi pamoja na wafanyakazi wengine wa TRA wakijitambulisha kwa wafanyabiashara wa Mwenge
Mr. Evarist Munishi akielezea aina mbalimbali za mashine za kutolea risiti Electronic Fisco Devices (EFD) na namna zinavyofanya kazi na ni wafanyabiashara wa aina gani wanatakiwa kuwa na mashine zipi kulingana na aina mbalimbali za biashara
WAFANYA biashara wakifuatilia kwa makini
Maofisa wa TRA wakiwa meza kuu pamoja na viongozi wa wafanya biashara wa Mwenge
Baada ya kupata elimu, mashwali na kero mbalimbali kutoka kwa Wafanyabiashara wa Mwenge zilitolewa
Samweli wa Street Winners Boutique akitoa kero zake
Bi Rehema akijibu maswali ya wafanya biashara
Leo maofisa wa TRA wamekutana na wafanya biashara wote wa Mwenge na kutoa mafunzo kuhusu wajibu wa mlipa kodi na hasa elimu kuhusu mashine mpya za risit EFD). pamoja na hayo wametueleza ni wakati gani mfanyabiashara anatakiwa kulipa ongezeko la thamani (VAT) au kulingana na kiwango chake cha biashara au kwa kushauriwa na maofisa wa TRA.
Imeonekana kwamba wafanya biashara wengi wa mwenge wamelazimishwa kuingia katika kulipa VAT wakati wao wenyewe bado ni wafanya biashara wadogo wasiostahili kuingia katika VAT. Kutokana na maswali mengi ya wafanya biashara, elimu ya kuingia kwenye VAT bado ni ndogo na si hivyo tu, wengi wa wafanyabiashara nikiwemo mimi, tunanunua bidhaa kutoka kariakoo bila kupewa risiti za VAT. Sasa mfanya biashara atalipaje atalipaje VAT wakati amenunua bila VAT?
Wafanyabiashara hao wamewashauri TRA kuhakikisha kwamba kule tunakonunua mizigo yetu kwa ajili ya kuja kuchuuza wawe wamehakikisha wanatoa risiti.
Jambo lingine ambalo ilielezwa kwamba litaendelea kumdidimiza mfanya biashara wa Kitanzania ni soko la ushindani. mathalani muuza simu wa Mwenge ni lazima aende kariakoo kwa wauzaji wa jumla ili anunue simu na aje kuiuza kwa kuweka faida. pamoja na kumuuzia bila risiti lakini pia mfanhya biashara huyohuyo wa jumla wa kariakoo anauza pia kwa rejareja ambapo bei yake inakuwa nafuu kuliko mchuuzi wa mwenge. Kwa maana hiyo,mfanyabiashara wa mwenge ataonekana ana bei kubwa hivyo mnunuzi kwenda kariakoo kununua kwa bei poa. Hivyo, mfanya biashara wa jumla awe ni wajumla tu na asiruhusiwe tena kuuza kwa rejareja ili kuwe na uwiano sawa.
Elimu ya kodi kwa walaji bado haitoshi. Wananhi wote wanatakiwa kueleweshwa na kufundishwa umuhimu wa kudai risiti na umuhimu wa kulipa kodi
TRA wanamjalije mfanya biashara ambaye kimsingi ndiye anayelipa kodi au wakala wa kodi? (VAT)
TRA inawazuiaje wafanya biashara wasio rasmi wanaoweka biashara zao barabarani au mbele kabisa ya duka ambalo linalipa kodi? Ikumbukwe kwamba machinga halipi kodi yapango, wala TRA hivyo bei za bidhaa zake zitakuwa nafuu zaidi na kulazimu walaji kununua kwao.
TRA inahakikishaje kodi wanazotoa zinanufaisha umma wote? Kuhakikisha wafanya biashara wanafanya biashara katika mazingira safi, parking ziwepo, mitaro iwe safi? Kama mlaji mwenye gari akitaka kununua kitu Mwenge akakosa parking ataenda mlimani City ambapo pana parking nzuri na safi. Hivi leo mitaa ya mwenge imejaa majalala kila mahali na ukiuliza unaambiwa ni miradi ya watu. Nitafanyaje biashara wakati mbele ya duka langu kuna jalala?
Imeelezwa pia kwamba mashine za kutolea risiti zitatumika kwa kila mfanya biashara kadiri muda unavyokwenda. wafanya biashara wameiomba Serikali itoe mashine hizo bure kwani kwa sasa zinauzwa ghali sana kiasi cha kushindwa kuzinunua. Kama mfanya biashara aliyeingia kwenye VAT ni wakala wa kuisaidia Serikali kukusanya kodi, basi wapewe nyezo bure ikiwa ni pamoja na hizo mashine, elimu ya kuzitumia na kuzifanyia matengenezo pindi zinapoharibika.
Na mdau Bahati
No comments:
Post a Comment