Maiti zikitapakaa nje ya Club hiyo
Wanajeshi wakisaidia kuchukua miili ya waliokufa katika ajali hiyo
Mama akiwa hataki kuamini anachoelezwa kwamba mpendwa wake amefariki
Moto ukionekana kwa nje
Wa kukkimbia haya, wa kuokoa wenzao haya, wa kushangaa nao wamo
Hakuna aliyejali kukaa karibu na maiti au karibu na wanaokata roho maana ilikuwa vurugu tupu
Magari ya Zimamoto yalijaribu kufanya kilichowezekana
Simanzi kwa kila mtu
Kabla ya moto kuzuka, ukumbi ulikuwa umelipuka kwa burudani za ukweli
Ukumbi ulikuwa umejaa sawasawa
Rais wa Dilma Rousseff akihutubia taifa huku akipambana na machozi yaliyokuwa yakikatiza hotuba yake
Zaidi ya watu 232 wamekufa baada ya club moja ya usiku ijulikanayo kama Kiss Night Club kuwaka moto baada ya cheche zilizotokana na michezo ya moto (fireworks) zzilizosababishwa na bendi iliyokuwa ikitumbuiza katika ukumbi huo wa starehe. Watu wengi walikufa kutokana na kuvuta hewa ya moshi iliyokuwa imetapakaa katika ukumbi huo. Katika ukumbi huo kulikuwa na mlango mmoja tu wa kutokea hivyo kufanya watu wengi washindwe kutoka nje haraka.Police Major Cleberson Braida Bastianello amesema kuwa wamehesabu miili ya watu 232 hadi sasa na miili hiyo imewekwa katika sehemu ya mochezo kwenye mochuari za dharura ili waweze kutambuliwa na ndugu zao.
Pamoja na magari ya zimamoto na ambulances kuwahi haraka, lakini moto pia ulikuwa umetapakaa haraka sana hivyo kushindwa kuokoa watu wengi.
"Bendi ilikokuwa ikitumbuiza ilianza kupiga mafataki kuelekezeaa kuu. Mara ceiling ikashika moto kidogo, mara moto ukaenea kwa kasi ya ajabu" alisema Pereira mmoja wa manusura wa ajali hiyo"
Baada ya watu kuona moto na moshi kila mtu alipaniki na kuanza kukimbia huku na kule kwa kugonganagongana tu humo ndani bila kutoka nje
No comments:
Post a Comment