Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa kuendelea na semina,
leo kwenye Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma.
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dk. Ali
Mohamed Shein na Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip
Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa
semina iliyoanza jana, na kuendelea leo kwenye ukumbi wa White House,
Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Pamoja naye ni Dk. Sheni na Kinana
HII UNAONAJE? Mjumbe wa NEC, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe akiteta jambo na Mzee Mtandika
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, ambaye sasa ni Mjumbe wa NEC, William
Mukama akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzake wa NEC Profesa Juma
Kapuya ukumbini
Wajumbe wa NEC Profesa Anna Tibaijuka na Mzee Mtandika wakibadilishana mawazo ukumbini
TUKIFANYA HIVI MAMBO YATANYOOKA AU SIYO? Inaelekea ndivyo Dk. Asha-Rose
Migiro alivyokuwa akisema kumwambia Nape katika mazungumzo yao ukumbi
kabla ya kikao
HAPO VIPI? Katibu wa Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib anaonekana
kumuuliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati
wakibadilishana mawazo kabla ya kikao kuanza
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro
akichati jambona Mjumbe wa NEC, Samwel Sitta na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye kabla ya kikao
Nape (kulia) akichangia kwenye mazungumzo hayo kati yake na Dk. Asha-Rose na Sitta
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Katibu wa
NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji, kabla ya kuanza kikao hicho leo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisahuriana jambo ukumbini na
Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye, kabla ya kikao kuanza leo
Wilson Mukama akiteta naMjumbe wa NEC, Steven Wasira nje ya ukumbi
Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akimsalimia Katibu wa NEC Siasa ana
Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro kabla ya kikao kuanza
ukumbini. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Vuai Ali Vuai kabla ya kikao
kuanza
Dk. Asha-Rose Migiro akishauriana jambo na Nape
SALAMU! Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa, Alhaj Abdallah Bulembo
akiwasalimia wajumbe wenzake wa NEC ukumbini kabla ya kikao kuanza
Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal (kulia) na Waziri Mkuu Mizengo
Pinda wakiwa safu ya mbele na baadhi ya wajumbe kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakisubiri kwa hamu kikao kuanza
Baadhi ya wajumbe wakipitia nyaraka muhimu kabla ya kikao kuanza
ENZI ZETU ZA IGUNGA VIPI? Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu
Nchemba anaonekana kumuuliza swali hilo Mjumbe wa NEC, aliyekuwa mbunge
wa Igunga Dk. Kafumu walipokutana nje ya ukumbi kabla ya kikao
kuanza
Wajumbe wa NEC wakiangua kicheko cha kutaniana kaba la kuingia
ukumbini. Kutoka kulia ni Dk. Rafael Chegeni, Januari Makamba,
Halimenshi Mayonga na Samwel Sitta.Picha Zote na Bashir Nkromo-Idara ya itikadi na Uenezi-CCM
No comments:
Post a Comment