Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akimfariji mmoja kati ya abiria waliokua katika Jahazi la Sun Rise, Juma Ali Jaku , iliyopata ajali na kuzama kati
ya Tanga na Mkokotoni karibu na Mkondo wa Nungwi, ikiwa imebeba jumla
ya abiria 32 kati ya hao 21 wameokolewa na 11 kati yao hadi sasa
hawajapatikana. Kushoto kwa Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pemba Juma Khamis.
Nahodha wa Jahazi ya Sun Rise, iliyozama
kati ya Tanga na Mkokotoni, karibu na Mkondo a Nungwi, Abdulla Saleh,
akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,
jinsi mkasa huo ulivyowatokea na kuzama baada ya chombo chao kupatwa na
dhoruba kali.
---
Nahodha na abiria mmoja ambao ni miongoni mwa watu
21 walionusurika kufa kati ya 32 waliokuwa wakisafiri na Jahazi
lililopata ajali na kuzama liitwalo Sun Rise likitokea Mkoani Tanga kuja
Mkokotoni Unguja, wakiwa katika wodi ya Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini A iliyopo Kivunge, Zanzibar wakiendelea kupatiwa matibabu.
Jumla
ya abiria 21 wameokolewa katika ajali hiyo na kupelekwa Kivunge kwa
ajili ya kupatiwa huduma ya matibabu ambapo hadi sasa abiria saba watoto
wakiwa watatu na watu wazima wane bado hawajapatikana kutokana na ajali hiyo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na
Viongozi wa Juu wa Ofisi yake ambayo ndio inayoratibu masuala ya maafa
walifika Hospitali ya Kivunge kuwapa pole majeruhi hao waliobakiwa
wakipatiwa huduma za Matibabu.
Nahodha
wa Jahazi hiyo Bwana Abdulla Saleh akiwa pamoja na Majeruhi mwenzake
Bwana Ali Juma Jaku alimueleza Balozi Seif kwamba ajali hiyo ilitokea
kutokana na kuchafuka mara Moja hali ya Bahari.
Nahodha
Abdulla alisema chombo chao chenye uwezo wa kubeba abiria 50 kiliondoka
bandarini Tanga salama Majira ya Saa nane za Usiku na walianza kupata mitihani na kuzama mara baada ya kuchafuka kwa bahari majira ya saa 11 za alfajiri.
Akiwapa
pole majeruhi hao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar Balozi Seif alisema
juhudi alizoonyesha Nahodha huyo katika kusaidia uokozi huo zinastahiki
kupongeza na Jamii yote.
Balozi Seif
aliwaombea majeruhi hao kupoa haraka na kuungana na familia zao na
kuutaka Uongozi wa Hospitali ya Kivunge kuendelea kuwachunguza Mareruhi
hao kutokana na juhudi kubwa waliyoifanya ya kusaidia harakati za uokozi
wa wenzao uliopelekea kupoteza nguvu nyingi.
Jahazi
hilo la Sun Rise lililokuwa likitokea Tanga kuja Mkokotoni mbali ya
kuchukuwa abiria pia lilibeba sanduku nne za maziwa pamoja na Polo zipatazo 30 za Mkaa.
Othmna Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment