WAKATI kukiwa na taarifa kwamba maofisa wa Shirika la
Upelelezi la Marekani (FBI) wametua nchini kwa ajili ya kufanya upelelezi wa
mauaji ya Padri Evarist Mushi, Jeshi la Polisi limetangaza dau la Sh10 milioni
kwa atakayefichua aliyemuua padri huyo.Padri Mushi aliuawa
kwa
kupigwa risasi Jumapili iliyopita wakati akienda
kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Teresia lililopo Beit el Ras nje
kidogo ya mji wa Zanzibar, ambapo inadaiwa kuwa waliomuua walikuwa wamepanda
pikipiki aina ya Vespa na walimfyatulia padri huyo risasi tatu akiwa ndani la
gari yake.
Wakati polisi wakitangaza dau hilo, Sheikh Ali Khamis
Ali (65) mkazi wa Kitope Kaskazini Unguja, aliuawa jana kwa kukatwa mapanga
mjini Zanzibar, baada ya wezi kuvamia shambani kwake.
Habari za kuaminika zilizopatikana juzi zinaeleza kuwa
maofisa hao wa FBI, wako nchini na tayari na wamekutana na baadhi ya viongozi wa
Serikali kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.
Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa maofisa hao
walikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kwa ajili ya
kuangalia ni namna gani watafanya shughuli zao katika upelelezi
huo.
Pamoja na ushiriki FBI, taarifa zinaeleza kuwa maofisa
wa Serikali ya Tanzania wamezungumza na taasisi za upelelezi za nchi tano, ili
kuongeza nguvu katika upelelezi huo.
Taasisi nyingine inayotajwa kuwa huenda ikashiriki
katika uchunguzi huo ni Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Uingereza
(Scotland Yard).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima
alilithibitishia gazeti hili kwamba Serikali imeanza kufanya mazungumzo na
mashirika mbalimbali ya upelelezi duniani kwa ajili ya kushirikiana nayo
kuchunguza mauaji ya Padri Mushi, lakini akasema kuwa ni mapema mno
kuyataja.
“Tumefuata maagizo aliyotoa Rais Kikwete kwamba
tushirikishe mataifa mbalimbali kuchunguza mauaji yaliyotokea Zanzibar, siwezi
kutaja kwa majina, ila tayari tumeanza kuzungumza na nchi mbalimbali,” alisema
Silima.
Akizungumza mjini Zanzibar jana, Kamishna wa Polisi
visiwani humo, Mussa Ali Mussa alisema kuwa hadi sasa hakuna mtu aliyefikishwa
mahakamani kuhusiana na tukio hilo la mauaji.
“Hakuna aliyefikishwa mahakamani, lakini wapo watu
ambao wamekamatwa wakihusishwa na tukio hili na tunaendelea kuwahoji, wengine
tunawaachia,” alisema na kuongeza:
No comments:
Post a Comment