Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua juu ya jeneza la
Marehemu Mzee Amos Kaguta(97),Baba Mzazi wa Rais Wa Uganda Yoweri Kaguta
Museveni wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika katika kijiji Cha
Rwakitura nchini Uganda.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa
Uganda wakiweka udongo kwenye kaburi la Mzee Amos Kaguta(97) wakati wa
mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akimpa pole Rais Yoweri Kaguta Museveni
kutokana na kifo cha Baba yake Mzee Amos Kaguta, katika kijiji cha
Rwakitura nchini humo.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akifariji mke wa Rais wa Uganda Mama Janet
Museveni kufuatia kifo cha Baba wa Rais Museveni Mzee Amos Kaguta.Picha na Freddy Maro-IKULU
--
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana aliungana na mamia ya wananchi wa
Uganda katika kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97) Baba ya Rais
Yoweri Museveni wa Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha
Rwakitura,magharibi ya Uganda.
Rais
Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa
Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa cnhi za Maziwa
Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Akitoa
salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa
Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na
kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na
kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea
marehemu.
Rais
Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo
alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuthamini elimu ambapo
aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali
kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee
wengi wenye umri wake.
Rais
Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao
ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa
kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe
akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana
na changamoto nyingi katika maisha yao.
Marehemu Mzee Amos Kaguta
alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini
Uganda. Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi
Vuai
Nahodha waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo
No comments:
Post a Comment