Taarifa hii inapitikana kupitia mtandao wake wa Facebook na inasomeka kama ifuatavyo;
Habari
zenu, mabibi na mabwana, marafiki zangu wa kwenye mtandao na wale wasio
marafiki zangu ambao naamini kwa namna moja au nyengine mtakapo soma
habari hii mtaipeleka kwa jamaii inayowazunguka ili kuweka hali vizuri .
maisha
ni kuhangaika na kwamba inataka mtu anayefahamu njia sahihi kuweza
kujua kuwa nikitumia njia hii hali itakuwa sawa na pengine mambo yangu
yatanyooka.hii inaweza kuwa ndiyo maana halisi ya hangaika ufanikiwe.
lakini tafsiri hii haiwezi kuwa kutumia njia za kudhulumu, kukaba, kuiba
au kufanya utapeli ili ufanikishe malengo yako mabaya dhidi ya mtu au
kikundi fulani cha watu.
hivi
karibuni nimekuwa napokea sana emails, sms, na hata twitts juu ya kitu
kinachoitwa TANZANIA LOAN SOCIETY, ambacho kwa namna moja au nyengine
kinaonekana kuwa ni mradi ambao umeanzia katika mikono ya Raisi Barack
Obama kuja tanzania kupitia Raisi Dr. Jakaya Kikwete na sasa mie
nikishirikiana na Waziri Mkuu Bwana Mizengo Kayanza Pinda
tunauendesha.Jambo ambalo si la ukweli hata kidogo na naomba tumia
nafasi hii kulikanusha kabisa mbele ya umma wa watanzania na wale wote
ambao kwa namna moja au nyengine wanafuatilia ninavyotuma kwenye kurasa
hii.
kwa
masikitiko makubwa sana napenda kuweka hadharani kuwa JAMBO HILI SI LA
KWELI na kwamba HAKUNA KITU na kwa yeyote ambaye atakuwa ametoa hela
yake basi atakuwa AMETAPELIWA.
kwa
upande wangu niwaombe ndugu zangu na vijana wenzangu watanzania kuwa
makini sana na mambo haya ya mitandao. maana wanaotangaza vitu kama hivi
wanaweza kuwa na nia mbalimbali ikiwemo, KUTUMIA JINA LANGU ILI
KUWAIBIA WATU, lakini pia KUTUMIA JINA LANGU ILI KUNICHAFUA, au kutumia
NJIA HII IIKIWA NI SEHEMU YA KUJIPATIA KIPATO KISICHO HALALI.
Hivyo
ni ushauri wangu kwenu vijana wenzangu ambao ninaamini kuwa mliamini
kuwa jambo hili ni ukweli kuacha kuamini vitu mnavyoviona pasi kuwa na
taarifa za uwakika.tuwe wepesi wa kuuliza kabla hatujajaribu maana
VYENGINE NI SUMU NA HAVIONJEKI.
Nimalize
kwa kuwashukuru wote ambao kwa namna moja au nyengine wamekuwa
wakinipigia simu kunijulisha na hata wale walioandika ujumbe mfupi wa
maneno pia. pia kuwapa pole wote ambao kwa namna moja au nyengine
wameathiriwa na zoezi hili. lakini haukuwa nia yangu kuona dhuruma hii
ikitokea ila ni ukweli kuwa lazima uelewe vizuri kuwa uchunguzi wa kina
lazima ufanyike na kujiridhisha pasipo kukurupuka maana unaweza fanya
jambo kumbe ndiyo unalikuza. lakini pia niwaombe wale ambao kwa namna
moja au nyengine kurasa zao za face book zimetumika kurusha matangazo
haya ya kiutapeli waone jinsi gani wanaweza kulizungumzia jambo hili ili
kuwasaidia wengi ambao wameathirika na imani yao juu ya hili
MIMI NDUGU YENU
RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE
AKHSANTENI KWA KUSOMA TAARIFA HII.
No comments:
Post a Comment