DR Shein akihutubia wana CCM katika Kusheherekea miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shain amewatoa
mashaka
WATU wanaohoji kutokuwepo kwa hati halisi ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar na kusema hati hiyo ipo na iwapo hawaamini wanaweza kwenda
Umoja wa Mataifa New York.
Amesema
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar chimbuko la kuasisiwa kwake
kulitokana na ridhaa ya wananchi wa pande mbili za Muungano na kuwataka
wanaowababisha wananchi kwa maneno ya mitaani kuacha kufanya hivyo kwa
sababu kila swali lao lina jawabu lake.
Dk
Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyeki wa CCM Zanzibar amesema kuundwa kwa
Muungano halikuwa ni jambo la kubahatisha bali lina malengo
yaliokusudiwa kabla ya kupatikana Uhuru ya Tanganyika mwaka 1961 na
kufanyika kwa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar Januri 12,1964.
Amesema
wenye wasiwasi na kutokuwepo kwa hati ya Muungano wamfuate ikulu
awaonyeshe chumba walichokutana Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid
Karume na kufanya makubaliano ya mwisho kabla ya kuunganisha nchi zao
Ameeleza
kuwa madhumuni ya vyama vya TANU na ASP yalilingana tokea vyama hivyo
vikiwa katika harakati zake za kujikomboa hivyo kurahisisha hata kazi ya
kuziunganisha nchi hizo mwaka 1964 pia vyama hivyo na kuzaliwa kwa CCM
mwaka 1977.
Aidha
Makamo huyo Mwenyekiti wa CCM amewaeleza wananchi kuwa Mapinduzi ya
Zanzibar ndiyo Uhuru kamili wa visiwa vya Unguja na Pemba huku akiwataka
wananchi kutowasiliza watu wanaopotosha ukweli na kuwataka kuacha
kufanya hivyo.
Dk
Shein amesema watu wanaobeza ukweli huo hawana nguvu ya hoja bali wana
lengo la kuwagawa wananchi ili waweze kuyafikia matarajio yao ambayo
amesisitiza yanapaswa kupuuzwa na kila mpenda amani na umoja.
Amewataka
watu hao kupuuzwa kwasababu hawajui wafanyalo na kwamba wanamangamanga
ili kutaka kuwagawa wananchi bila ya kufikiri kwa makini .
Akizungumzia
faida za Muungano Dk Shein amesema kiuhalisia wananchi wa Zanzibar
ndiyo wanaofaidika na Muungano huo kwani kila uendepa katika Tamnzania
Bara kuna wazanaziabri waliotamalaki na kuwekeza miradi na mitaji .
Alisema
Zanzibar inafaidika na siko la Bara ambapo kabla ya Mapinduzi ilikuwa
ikiagiza bidhaa za vyakula na mahitaji mengine kutoka nchi za Pakistan,
Japan na mashariki ya mbali jambo ambalo sasa linapatikana kutoka Mikoa
ya Bara
Kwa
upnde wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizunguimza
kabla ya kumkaribisha Dk Shein ,amesema nguvu ya umoja na maelewano
kati ya visiwa vya Unguja na Pemba inatokana na kuwepo kwa Muungano na
kusema nje ya jambo hilo lolote linaweza kutokea.
Vuai
amesema Muungano wa Tanzania licha ya kuleta tija za kiuchumi lakini
pia kwa kipindi chote cha miaka 49 ya kuwepo kwake umelinda na kusimamia
usalama wa raia na mali zao.
Amesema
hata pale Tanznia ilipovamiwa na majeshi ya Idd Amini mwaka
1978,wanajeshi wa Zanzibar waliingia vitani ili kuihami nchi yao
vikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba na kwamba nje ya Muungano umoja huo
unaweza kuparaganyika .
Naibu
huyo Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,amesema CCM itaendelea kujivunia
matunda ya TANU na ASP kutokana na kupigania kwao maslahi ya watu
waliokuwa wakikandamizwa na kubaguliwa katika ardhi ya nchi zao.
Amesema
vyama hivyo kwa pamoja vilihakikiisha vinajenga misingi imara ya
heshama na utu kwa kila binadamu na kuondosha matabaka,ubaguzi wa rangi
na maonevu hadi pale vilipoamua kuunganisha nguvu zake na kuzaliwa kwa
Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977.
No comments:
Post a Comment