Waziri
wa elimu wa Ujerumani, Annette Schavan, amevuliwa cheo chake cha
Daktari wa Falsafa, baada ya kugundulika kuwepo na wizi wa mawazo ya
mtu.
Chuo
Kikuu cha Düsseldorf kilichoko mashariki wa Ujerumani, kimesema jana
jioni kuwa Schavan hakuonyesha vyanzo ipasavyo katika shahada yake ya
juu ya mwaka 1980, ambayo ilichunguza uundwaji wa dhamira na kwamba kwa
maksudi alichukuwa mawazo na kuyaonyesha kama ya kwake.
Madai
kuwa Schavan aliiba mawazo ya sehemu ya shahada yake ya juu, yalianza
mwaka uliyopita, wakati madai yasiyo na jina yalipochapishwa kwenye
mtandao wa intaneti.
Schavan
siyo mwanasiasa wa kwanza maarufu nchini Ujerumani kudaiwa kuiba mawazo
mwaka 2011, aliyekuwa waziri wa ulinzi Karl-Theodor zu Guttenberg
alivuliwa shahada yake ya juu na kulaazimishwa kujiuzulu.
No comments:
Post a Comment