Rais Mugabe amewekewa vikwazo vya kusafiri katika nchi za Ulaya tangu mwaka 2002 lakin kwa mara nyingine tena amekiuka kwa kutumia haki yake kama Mkatoliki kuhudhuria misa ya kuapishwa kwa Papa Francis Kesho Jumenne. Pamoja na kwamba Mugabe amepitia kiwanja cha ndege cha Italia lakini alipokelewa na padre ambaye alitumwa na Papa na kumpeleka rais Mugabe kwenye hotel maalum (Via Veneto) Hata hivyo taarifa kutoka Vatican zinasisitiza kwamba Vatican haijamwalika mtu yeyote binafsi, ila imewaalika watu wote na hakuna mtu yeyote atakayepeaw kipaumbele dhidi ya mwingine. Hata hivyo Mugabe anajivunia Papa Francis kwa kuwa yeye ni mmoja ya watu waliosoma katika shule za Jesuit shirika ambalo Papa Francis ni mtu wao.
Ma Ying-jeou rais wa Taiwan
Taiwan in uhusiano wa kidiplomasia na nchi moja tu ya ulaya ambayo ni Vatican. Hata hivyo China inapinga uhusiano wa kidiplomasia kati ya Taiwan na VAtican na China imeweka sharti ya kuhamisha ofisi za balozi wa Papa kutoka Taipei (taiwan) kwenda Beijing na pia papa asiwe na ruhusa ya kuteua maaskofu wa kichina. Ruhusa ya kuteua maaskofu wa kichina ifanyike tu na baraza la maaskofu wa china ambalo liko chini ya Chama cha kikomunist cha China.
Cristina Fernández. Rais wa Argentina
Enzi hizo huko Argentina
Akiwa Kardinali, aliwaita marais na wanasiasa wa argentina na kuwakaripia pale walipokosea kama anayvoonekana hapa akiwa ofisini kwake na rais wa sasa wa argentina
Leo Jumatatu Rais Cristina Fernández amewasili vatican na Papa Francis amempokea vizuri sana
Papa Francis akimbusu rais wake Cristina Fernández
Ni kwa mara nyingine tena Papa Francis ameendelea kudhihirisha kile anachosema kuwa kusamehe na kumpenda adui yako pale alipompokea rais wake wa Argentina ambaye mara kwa mara wamekuwa wakizozana sana kuhusu mambo mbalimbali. Rais Cristina pamoja na marehemu mumewe rais Nestor Kirchner walikataa waziwazi mafundisho ya kanisa katoliki ya kutoa mimba, kutumia madawa ya kuzuia mimba kubadili jinsia na ndoa za jinsia moja. Hayo yote yanafanyika kwa kuhalalishwa na wanasiasa wa Argentina na hii imekuwa nshi ya kwanza Amerika ya kusini kuhalalisha ndoa za mashoga. Papa Francis wakati huo akiwa kardinali alipambana na hali hii kwa nguvu zote na alikwaruzana sana na wanasiasa wa Argentina mpaka ikafikia mahali viongozi wa Argenitna wakawa hawahudhurii tena kanisani kama mgomo kwa kardinali ambaye aliwaita mafisadi na (demagoguery, totalitarianism)
Ecumenical Patriarch Bartholomew I
Patriarch Bartholomew I ni papa au kiongozi wa kanisa la mashariki. Huyu atakuwepo kesho na anakuwa kiongozi wa kwanza kutoka Istambul kuhudhuria sherehe kama hizi kwa zaidi ya miaka 1,000 iliyopita. Katika ibada ya kumsimika papa kutakuwa na mchangajiko wa liturgia ya magharibi na mashariki. Kwa mfano, Injili itaimbwa kwa kigiriki badala ya kilatiki akama ilivyozoeleka. Hata hivyo kabla ya ibada kuanza, Papa Francis na Patriarch Bartholomew wataenda kufanya ibada katika altare kuu juu ya kaburi la mtume Petro.
Viongozi wengine wakuu wa madhehemu 33 yakiwemo yale ya Kikristo, Budha, Islam, Wayahudi, Sikh na Jain wamethibitisha kuhudhuria ibada hiyo
Viongozi wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani watakutana Vatican kesho kwa ajili ya kuhudhuria misa ya kunsimika Papa Fraicis.
Uongozi wa Italy umesema unatarajia watu milioni moja au zaid kuhudhuria shughuli hiyo.
No comments:
Post a Comment