Na:Hussein Makame na Genofeva Matemu-Maelezo
WAZIRI
wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Serikali inahitaji
injini za kisasa ili kuboresha usafiri wa treni kwa mkoa wa Dar es
Salaam na
reli ya kati kwa ujumla.
Dk.
Mwakyembe ameyasema hayo leo (jana) wakati akiongea na wajumbe wa
kamati ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea mradi wa reli wa
kusafirisha abiria jijini Dar es Salaam .
Alisema
kuwa iwapo injini hizo zitapatikana zitaipunguzia Serikali gharama
kubwa kwa kuwa zinatumia mafuta machache na zinakwenda kwa kasi na kutoa
faida mara tatu ya inayopatikana sasa kwani zinatumia vichwa viwili
vya treni na mabehewa nane kwa usafiri wa Dar es Salaam.
“Gharama
za injini hizi ni Dola za Kimarekani milioni 6 ambazo Serikali
imeshindwa kuzipata kutokana na uwezo mdogo wa kifedha iliyonayo .Hivyo
basi juhudi za pamoja zinahitaji baina yetu sote ili kuiboresha sekta
hii ambayo ni mhimili wa ukuaji wa uchumi wa nchi” , alisema Dk.
Mwakyembe.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Peter
Serukamba aliishauri serikali ijitahidi kuboresha mradi wa reli wa
kusafirisha abiria jijini Dar es Salaam ili kuongeza faida inayopatikana
katika huduma hiyo.
Naye
msemaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Midladjy Maez alisema kuwa
gharama za uendeshaji wa mradi huo ni kubwa, hivyo basi alipendekeza
kuboreshwa na kuimarishwa kwa njia za treni na kumalizia ujenzi wa vituo
vya stesheni za njiani.
Maez
alisema, “Kwa wakati huu TRL haiwezi kumudu gharama za uendeshaji wa
treni hii, kwa hiyo tunaiomba Serikali itoe ruzuku ili TRL iweze
kupunguza hasara inayoipata kila mwezi.
Wajumbe
wa kamati hiyo walifanya ziara ya siku moja ya kutembelea mradi huo ili
kuona maendeleo yake na changamoto zilizoko na kuona ni jinsi gani
wanaweza kuzitatua ili kuboresha huduma ya usafirishaji wa abiria kwa
kutumia reli.
No comments:
Post a Comment