ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Tuesday, March 19, 2013

Kesi ya mtoto wa Gadaffi yaunguruma Arusha




 Saif al-Islam Gaddafi
 

Mahakama ya Afrika inayoshughulikia haki za binadamu yenye makao yake jijini Arusha imeamuru  Serikali ya Libya kuendesha kesi inayomkabili mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gadaffi kwa uhuru na haki.
Saif al-Islam Gaddafi, ambaye ni mtoto wa pili wa Gadaffi amekuwa akishikiliwa na vyombo vya usalama vya Libya tangu Novemba 19, 2011 baada ya kukamatwa wakati akijaribu kukimbia nchi hiyo baada ya kuuawa kwa baba yake na kaka yake, Mtassim Gaddafi, Oktoba 20, 2011.
Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika yenye makao makuu mjini Addis Ababa, Ethiopia ndiyo iliyowasilisha shauri hilo kwenye Mahakama ya Afrika kwa kuwa Serikali ya Libya haijaridhia mikataba ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.
Kutokana na hali hiyo, hata familia ya Gadaffi ilishindwa kufungua kesi hiyo kwani taasisi au watu binafsi wa Libya hawana uwezo wa kisheria wa kufungua kesi kwenye mahakama hiyo kutokana na kikwazo cha Serikali yao.
Shauri hilo lenye namba 002/2012 lilisikilizwa na majaji kumi na moja walioongozwa na Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Sophia Akuffo kutoka Ghana, Ijumaa iliyopita.
Wengine waliokuwemo kwenye jopo hilo ni pamoja na Makamu wake, Jaji Fatsah Ouguergouz, Jaji Mkuu wa zamani, Augustine Ramadhan pamoja na Majaji Sylvain Ore, Duncan Tambala, Gerald Niyugeko, Bernard Ngoepe, Elsie Thompson, Hadji Guisse, Kimelabalou Aba na Ben Kioko.
Jopo hilo la majaji pia limeiamuru Serikali ya Libya kuruhusu ndugu, jamaa na marafiki wa mtuhumiwa huyo kumtembelea kipindi chote shauri dhidi yake linaposikilizwa.
Serikali ya Libya imetakiwa kutoa taarifa mahakamani kuhusu utekelezaji wa amri hiyo siku 15 tangu kupokelewa kwa nakala ya hukumu.
Familia ya Gadaffi imekuwa haifurahishwi na mwenendo wa kesi ya  Saif huko Libya.

SOurce: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...