ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, March 7, 2013

IRAN YATANGAZA VITA RASMI

 
   
 
 
 
 
 
 
 

Wakati mjadala mkubwa wa kutengeneza silaha za nyuklia ukiendelea duniani juu ya Iran, kuna maandalizi makubwa za vita vya kuangamiza panya nchini humo.
Nchini Iran Idadi ya panya hao wakubwa imekuwa kubwa kuliko idadi ya wananchi woe na wameleta kero kubwa kwa binadamu.
Panya hao wenye uzito wa zaidi ya paudi 11 wameshindikana kuuwawa baada ya kampeni ya kuwauwa kwa sumu kushindwa. Hivyo serikali jijini Teheran imeunda vikosi 40 vya walenga shabaha mahiri ambao kazi yao ni kuwavizia na kuwauwa panya kwa silaha za moto.

Walenga shabaha hao wanaotumia bunduki za rifles zenye mwanga wa infra-red wameshafanikiwa kuwauwa panya 2000 wiki iliyopita.
Katika jiji la Teheran lenye wakazi zaidi ya milioni 12 inakadiriwa panya wake kuwa na idadi ya mara mbili ya wakazi hao yaani milioni 24. Mamlaka za Miji mikubwa hasa Teheran zimeanza rasmi vita hivyo ambavyo wanafikiri vitaweza kuzaa matunda ya kuwaangamiza panya hao.
Vita vyetu vya kupambana na mbu waenezao malaria ni vya iaka mingi. Tuna cha kujifunza kwa wenzetu?


1 comment:

  1. kweli mdau inatisha panya kama mbwa sasa ningekua nimimi nisinge fuga mbwa watati kupanya wakubwa nawanafaa kulinda

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...