KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Waziri
anayeshughulikia mambo ya chama katika Chama Cha Kikomunisti cha China,
Wang Jiarui, alipokutana naye leo Machi 20, 2013, kwenye Ofisi za CPC,
mjini Beijing, China na kuwa na mazungumzo naye. Nyuma ya Kinana ni
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na waziri
anayeshughulikia masuala ya chama wa Chama cha Kikomnisti cha China,
Wang Jiarui, alipokutana naye leo Machi 20, 2013, kwenye Ofisi za CPC,
mjini Beijing, China.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipewa zawadi ya pambo la
Kichina, na Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo
mjini Beijing, Xiong Weiping, Kinana alipotembelea kampuni hiyo na
ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya mafunzo
nchini China. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,
Dk. Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa zawadi ya kinyagoo cha
Kimakonde cha aina ya 'Ujamaa', Rais wa kampuni ya Aluminum ya China
(CHINALCO) kilichopo mjini Beijing, Xiong Weiping, alipotembelea kampuni
hiyo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya
mafunzo nchini China.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitia saini kweneye kitabu
maalum cha wageni, katika kampuni ya Aluminum ya China ((CHINALCO).
Kushoto ni Rais wa Kampuni hiyo, Xiong Weiping na wapili kushoto ni
Katibu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Khamis Suleiman Dadi.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) akitazama baadhi ya
malighafi, alipotembelea kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO),
alipotembelea kiwanda hicho mjini Beijing, Machi 20, 2013. Wapili kulia
ni Rais wa Kampuni hiyo Xiong Weiping .
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiwa katika
mazungumzo na uongozi wa CHINALCO, Kinana na ujumbe huo walipotembelea
kampuni hiyo wakiwa katika ziara ya mafunzo Beijing, China.Picha na Bashir Nkromo
No comments:
Post a Comment