Miss
World Africa 2005, Nancy Sumari leo amezindua kitabu chake cha watoto
kiitwacho Nyota Yako. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu wakiwemo mamiss Tanzania wa
zamani, Jacqueline Ntuyabaliwe na Faraja Nyalandu.
Wengine ni pamoja DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya watoto na Makamu Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Profesa Esther
Mwaikambo, Jokate Mwegelo, Shaa, Ally Remtullah. Fina Mango na wanafunzi
mbalimbali.
Akizungumzia jambo lililomsukuma kuandi ka kitabu hicho, Nancy alisema:
Vilinisukuma vitu vingi, kwanza nafasi ya mwanamke kwenye jamii yetu,
umuhimu wake, sababu ya kumuenzi na kumsherehekea na kutambua michango
yetu, mwanamke mdogo, msichana mdogo, mama zetu, bibi zetu. Kuna kila
sababu ya sisi kuangaliana na kutambuana na pia kufananisha.
Profesa Mwaikambo akikielezea kitabu hicho
Profesa Mwaikambo akimuonesha picha ya kwenye kitabu hicho mtoto wa Nancy, Zuri
Sababu baada ya kutembea kwenye shule nyingi na kuzungumza na
wasichana wengi nimegundua kwamba story zetu zinafanana. Changamoto ni
nyingi tunazozipitia na tunafanana kwa vitu vingi kwahiyo nikaona ni
vyema nikawafananisha wasichana wengi wakamwangalia mwanamke kama Dokta
Migiro wakasikiliza story yake, wakajiona kwenye hiyo hadithi, wakaona
uwezo wao wa kufikia alipofikia Dokta Migiro.
K-Lyinn akisaini kitabu cha waliohudhuria uzinduzi huo
MC wa uzinduzi huo Rebeca Gyumi
Ally Remtullah
K-Lyinn akifuatilia kwa ukaribu uzinduzi
Faraja Nyalandu
Nancy aliongeza kuwa mwanae pia alimchochea kuandika kitabu hicho.
“Baada ya mimi kuwa na Zuri nikaona kuna umuhimu wa yeye kuangalia
wanawake wa kitanzania kama role models. Anaweza akawaangalia
wanaojulikana akawajua pia lakini kuna kila sababu ya kuangalia wanawake
wengi na michango mingi inayofanyika kwenye jamii yake akawatambua
wanawake na kuwaenzi.”
Kuhusu upatikanaji wa kitabu hicho, anasema, “kwanza nitakisambaza
kwenye shule za msingi bure, halafu nitakisambaza kwenye bookshop ambako
kitauzwa, kwahiyo watoto wa shule ya msingi watakuwa na access nacho
bure lakini wengine wengi watakinunua kwenye bookshop. Hizo hela ambazo
zitapatikana zitaprint kitabu na kukisambaza mbali zaidi.”
“Nimepata mchango mkubwa sana kutoka Bongo5 Media Group ambao
wamenisaidia kufanikisha kitabu hiki, nawashukuru sana,” alisema Nancy.
Farja Nyalandu akizungumza
K-Lyinn akizungumza na Ally Remtullah
K-Lyinn
Kaka yake Nancy Sumari, Davis Abraham Sumari (kulia)
Fina Mango
Fina Mangi na Faraja Nyalandu
Akizungumzia kasumba ya watanzania wengi kutopenda kusoma vitabu na
jinsi alivyokabiliana nayo Nancy anasema, “nilimshirikisha mchoraji
mzuri sana kwasababu nilitaka kumvutia mtu kwa wepesi kwanza kiwe
kifupi, yaani kidogo. Ni kitabu ambacho unaweza kukipitia ndani ya
dakika tano. Kuna picha nyingi lakini meseji yake ni nzito sana.”
Kwa upande wake Profesa Mwaikambo(74), ambaye mwaka huu ubalozi wa
Marekani ulimtunuku tuzo ya haki ya Dk Martin Luther King amempongeza
Nancy kwa kuandika kitabu hicho na kusema kuwa watoto wengi hasa wenye
kuanzia umri wa miaka mitatu wataweza kukifurahiia kwa kuangalia picha
tu.
Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari King’ongo ya Kimara jijini Dar es Salaam
Shaa na Nancy wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi
Picha ya pamoja na Nancy, K-Lyinn, Ally Remtullah na rafiki
Nancy na Faraja
Mamiss Tanzania wa zamani wakiwa wameshikilia kitabu hicho
Mwanafunzi akifurahia kumsomea mzungu kilichoandikwa kwenye Nyota Yako
Alisema ubongo wa mtoto huanza kukua akiwa na umri wa miezi tisa na
akifikia mwaka mmoja unaweza kumfundisha chochote na akaelewa.
“Hakuna mtoto mdogo mjinga, hakuna, labda kama amezaliwa na mtindio
wa ubongo, lakini mtoto yeyote anayezaliwa na mwanamke ana akili za
kutosha kabisa lakini lazima awe exposed “alisema Profesa Mwaikambo.
No comments:
Post a Comment