Mtoto wa miaka 19 ametengeneza historia kwa kuwa mtoto wa kwanza Kenya kuwa Diwani akiwa na umri wa miaka 19 tu. Kibiwott Munge, ambaye amegombea kupitia chama cha URP, ameshinda katika jimbo la Lembus Perkera huko Baringo kwa kura 3,333 hivyo kumfanya aandike historia ya kuwa Mkenya wa kwanza mdogo zaidi kupata udiwani.
Kufuatia ushindi huu, watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa Sekondari aliyowahi kusoma iitwayo Tenges Boys High School, wanafunzi walishangilia kwa furaha kuu ushindi huu wa Kibiwott.
Kufuatia ushindi huu, watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa Sekondari aliyowahi kusoma iitwayo Tenges Boys High School, wanafunzi walishangilia kwa furaha kuu ushindi huu wa Kibiwott.
“Huu ni ushindi kwa vijana na hii inaonyesha kwamba vijana wana uwezo mkubwa wa kuiongoza nchi" alisema Mheshimiwa Munge katika hotuba yake ya kukubali matokeo hayo yaliyompa ushindi.
Hata hivyo, Mheshimiwa Munge amewashukuru wazazi wake kwa kumpa baraka zao na pia anamshukuru sana rafiki yake wa karibu Mr. Njoroge ambaye alimwazima pikipiki yake ambayo kijana huyu ndiyo aliyoitumia katika kampeni zake zote hadi kufanikiwa kuchaguliwa.
Mtoto huyu anasema kwamba alipata uzoefu na nia ya kuwa kiongozi wa kisiasa hsa kwa kusoma gazeti la Taifa Leo. Katika uwakilishi wake , Mheshimiwa Kibiwott Munge anaahidi kuwatetea vijana ili waweze kuwa na maisha bora.
Hii ni changamoto kwa vijana wetu wa Tanzania badala ya kulalamika tu tuamue na sisi kuchukua hatua za kugombea maadam katiba inaruhusu Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 anaweza kugombea, basi tutumie fursa zinazojitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali kwa nia ya kuleta mabadiliko ya kweli.
Uchaguzi kwa wenzetu wa Kenya ni kitu muhimu sana na tulishuhudia mwananchi mmoja akilia kwa uchungu sana baada ya jina lake kutoonekana katika karatasi ya kupigia kura. Alilia kwa uchungu kwa sababu kura yake moja tu ingeweza kuleta mabadiliko makubwa. 50%+1
Kwa hapa kwetu watu milioni 5 tu kupiga kura wakati wenye sifa za kupiga kura tunazidi milioni 20 ni vigumu kuleta mabadiliko tunayopigia kelele kila siku. Kura ndiyo msemaji au mkombozi wa mwisho wa matatizo yanayotuzunguka. Tusiwaache wachache watuamulie. Nafasi ya kuamua inapopatikana basi tuitumie kikamilifu.
Na mdau: Bahati
No comments:
Post a Comment