
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mhariri Mtendaji wa Habari
Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park
iliyopo mji wa Johannesburg, Afrika ya Kusini jana jioni.Kulia ni Katibu
mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya
kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu
wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete yupo Afrika ya Kusini kuhudhuria
Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika
mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi.Mkutano huo umeandaliwa
na Chama cha African National Congress(ANC).
Rais Jacob
Zuma wa Afrika ya Kusini akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
katika ukumbi wa Freeedom Park mjini Pretoria Afrika ya Kusini
kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyioshiriki katika harakati
za ukombozi Kusini Mwa Afrika.
Rais Jacob
Zuma wa Afrika ya Kusini(Katikati) akiongea na waandishi wa habari muda
mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Viongozi wa vyama vilivyokuwa
mstari mbele katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika leo
mchana.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa FreedomPark,Jijini
Pretoria Afrika ya Kusini. Kushoto ni Rais Jakaya Kikwete mbaye pia ni
Mwenyekiti wa CCM na kulia ni Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye ni
kiongozi wa ZANU PF.
Rais
Dkt.Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM akiwa katika picha ya
pamoja na Mwenyeji wake Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini ambaye pia
ni kiongozi wa ANC(Watatu kushoto), Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe
ambaye pia ni kiongozi wa ZANU PF(Wapili kushoto) pamoja na Waziri Mkuu
wa Namibia aliyeiwakilisha SWAPO, muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wao
uliofanyika katika ukumbi wa Freedom Park,jijini Pretoria nchini Afrika
ya Kusini kwa mwaliko wa chama tawala cha Afrika ya Kusini ANC.(picha
na Freddy Maro).
No comments:
Post a Comment