ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, March 27, 2013

MZUNGU NA DOLA FEKI
















Huyu Mzungu anayesumbua na dola zake feki analeta matatizo sana katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. 
Kama wiki moja iliyopita nilimzikia jirani yangu mwenye duka la nguo akilalamika kumwachia Mzungu akakimbia baada ya kununua nguo za kutoshakatika duka lake na kutoa noti za dola mia ambazo yeye alizigundua kuwa ni feki na hapo hapo mzungu huyo alitokomea haraka na tax aliyokuwa amekuja nayo.
Kwa bahati mbaya jana amekuja ofisini kwangu miida ya saa 2 usiku na kulalamika kuwa amechelea na beaural de change zote zimefungwa. Alimkuta kijana ambaye hata hivyo aliingia mtegoni baada ya kumpa $ 100 kwa rate ya 140,000 badala ya 160,000/= ambapo 20,000/= ingekuwa ni kwa ajili ya usumbufu. Kijana leo ameenda mlimani city kuchange ile dola ili arudishe 140,000 ya bosi wake na yeye apate 20,000 ya fasta fasta. Kijana alikwama baada ya dola 100 yake kutobolewa na hapo hapo amekutana na watu wengine wawili wakiwa na tatizo hilo hilo.
Watz tusiwaamini sana watu tusiowajua hata kama ni Wazungu. Wazungu wengi sasa hivi ni njaa tupu aheri tena ya sisi wabongo. Tusiwaamini kwa kuwa tunafikiri wana pesa nyingi ndo hawawezi kututapeli. Hawa jamaa wana utapeli mkubwa na hata mdogo. Ni njaa tupu na watatuumiza sana tusipoacha ulimbukeni na kuwa WEREVU. 
Mzungu huyu anapenda kufanya uhalifu wake miida ya jioni kwa kisingizio kwamba maduka ya kubadilishia pes yamefungwa. Au ananunua vitu vya gharama kwa kujifanya hana pesa za kibongo. Wako wengine wanavaa mavazi ya kipadre na kujiita wamisionari na kuchukua vifaa vingi kwa dola feki au kwa post dated check ambazo ni feki. 
Wakati huu ambapo Tanzania inaonekana kwa watu wa nje kuwa inaimarika kiuchumi, wanajua bado hatujaimarika kimaarifa, hivyo ulimbukeni na kukosa maarifa kutatuponza sana. Watu wenye biashara za m-pesa ni target kubwa. Usikubali kuuza bidhaa zako kwa dola, Euro au paund kama huna mashine ya kuzihakiki.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...