Aliyekuwa mjumbe wa baraza kuu
la Uvccm mkoani Arusha,Benson Mollel aliyevalia shati la kung’aa tofauti
na wenzake akitoa msaada kwa mtoto aitwaye frank wakati jumuiya hiyo
ilipofanya ziara ya kutembelea wagonjwa katika hospitali ya mkoa ya Mt
meru hivi karibuni enzi ya uhai wake,anayefuatia ni mwneyekiti wa uvccm
mkoani hapa,Robinson Meitenyiku
MJUMBE wa baraza kuu la umoja
wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa
Arusha ,Benson Mollel(26) amekutwa amefariki dunia ndani ya hoteli ya
Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na
Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.
Tukio hilo lililogusa hisia
za wengi lilitokea ghafla leo 3 /3/2013 majira ya saa 6:oo mchana
tayari limezua hali ya hofu na mashaka kwa wakazi wa jiji la Arusha na
viunga vyake ambapo tayari limehusishwa na hisia mbalimbali ikiwemo
kulishwa sumu kali.
Kabla ya kukutwa na umauti
alikuwa ni mwanasiasa mchanga ambaye pia alikuwa ni mfanyabiashara wa
madini mkoani hapa ambapo kifo chake kimehusishwa na masuala ya kisiasa
na kibiashara
Marehemu Mollel,aliutwaa
ujumbe wa baraza kuu la Uvccm mkoani Arusha mwaka huu huku akimrithi
mkuu wa wilaya ya Korogwe kwa sasa,Mrisho Gambo katika uchaguzi uliokuwa
na mshike mshike huku akitajwa kuwa kambi ya waziri mkuu
mstaafualiyejiuzulu,Edward Lowasa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya
habari ndani ya hoteli hiyo vimedai ya kwamba marehemu aliwasili mnamo
machi 2 mwaka huu majira ya usiku hotelini hapo akiongozana na mwanamke
mmoja aliyetambulika kwa jina la Nancy ambapo walichukua chumba nambari
214.
Mmmoja wa walinzi hotelini
hapo aliyejimbulika kwa jina la Obeid Mollel kutoka kampuni ya ulinzi ya
Victoria Support Services ambayo inaimarisha ulinzi hotelini hapo
alisema kuwa marehemu aliingia na mwanamke huyo na kisha kuondoka ghafla
kabla ya kurejea tena wakiwa wote usiku.
Hatahivyo,alisema kuwa wakati
wakiwa hotelini hapo marehemu aliomba kuegesha gari lake jipya ambalo
bado halijapata usajili lenye nambari 4093 gx 110 aina ya mark ii grande
ambapo alikubaliwa na kisha kurejea chumbani na mwanamke huyo ambaye
anatajwa kuondoka leo asubuhi 3/3/2013
Hatahivyo,majira ya asubuhi
mmoja wa wahudumu hotelini hapo(jina lake limehifadhiwa) alisema kuwa
mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maryam aliwasili hotelini
hapo majira ya saa 5;00 na kuomba kupelekwa moja kwa moja chumba
alichokuwepo marehemu.
Mhudumu huyo kwa sauti ya
upole alisema kuwa wakati mwanamke huyo akiomba kupelekwa chumbani hapo
marehemu naye alipiga simu mapokezi na kuomba mwanamke huyo apelekwe
chumbani kwake ambapo walitekeleza jukumu hilo.
Akiendelea kusimulia tukio
hilo mhudumu huyo alisema kuwa walimwona mwanamke huyo akitoka ghafla
nje ya hoteli hiyo majira ya saa 6;00 mchana bila kumtambua sura yake
ambapo hawakufuatilia chochote kwa kujua kwamba hakuwa na nia mbaya.
“Sisi baada ya kumwelekeza
Yule dada chumba alichofia marehemu hatukufuatilia hadi pale mlinzi
alipomwona akitoka tena nje ya geti wala hakukaa muda mrefu”alisema
mhudumu huyo
Hatahivyo,wakati hayo
yakiendelea mhudumu huyo aliamua kupiga simu ya chumba alichofia
marehemu ili kujua endapo ataendelea kukodisha chumba hicho ama la
lakini katika hali isiyo ya kwaida simu ya chumba hicho ilikuwa
haipokelewi.
Wakati hayo yakiendelea
alisimulia kwamba mmoja wa wahudumu ambaye alikuwa akifahamiana na
marehemu kwa muda mrefu aliamua kumpigia kupitia simu yake ya mkononi
lakini nayo haikupokelewa vilevile.
Baada ya hatua hiyo mhudumu
huyo aliamua kupanda ngazi kwenda chumbani kwa marehemu lakini katika
hali isiyo ya kawaida alikuta mlango ukiwa wazi na mara alipomwamsha
marehemu hakuweza kuamka na ndipo alipotoa taarifa kwa uongozi wa hoteli
na kisha kuviarifu vyombo vya usalama.
Hatahivyo,mhudumu huyo
alipohiojiwa na jamiiblog.co.tz alisema kwamba anahisi nini chanzo cha
kifo cha marehemu huyo alisema kuwa huenda mwanamke aliyekuwa naye
(Maryam) huenda alitekeleza mauaji hayo kwa ustadi mkubwa bila wao
kufahamu.
“Unajua vyumba vyote vya huko
juu ghorofani ukifunga mlango tu huku chini sisi mapokezi tunasikia sasa
cha ajabu mlango tumeukuta wazi na nahisi alitekeleza haya mauaji
akaona asifunge mlango kwa kuwa tutasikia”alisema mhudumu huyo kwa upole
Jeshi la polisi liliwasili
hotelini hapo majira ya saa 8;00 mchana na kuupakia mwili wa marehemu
kupitia gari lenye nambari za usajili 1477 na kisha kuufikisha katika
chumba cha kuhifadhia maiti ndani ya hospitali ya mkoa ya Mt,Meru
Akizungumza katika eneo la
tukio mkuu wa jeshi la polisi wilayani Arusha,OCD Gilles Muruta alisema
kwamba jeshi la polisi bado linachunguza undani wa tukio hilo kwa kuwa
limejitokeza ghafla na hapo baadaye litatoa taarifa mwa vyombo vya
habari.
Hatahivyo,katibu mwenezi wa
CCM mkoani Arusha,Isaack Kadogoo alisema kuwa wao wamepokea tukio hilo
kwa mshtuko mkubwa kwa kuwa bado wamepigwa na mashangao kwa jinsi namna
lilivyotokea.
Baadhi ya wanasiasa wa vyama
mbalimbali vya siasa pamoja na wafanyabiashara wa madini mkoani Arusha
waliwasili eneo la tukio nje ya hoteli hiyo ambapo wengine walishindwa
kujizuia na kujikuta wakiangua kilio nje ya hoteli hiyo.
Baadhi yao,James ole Milya
kada wa Chadema pamoja na Mathias Manga diwani wa CCM kata ya Mlangarini
wanaotajwa kuwa karibu na marehemu wakati wa uhai wake walionyeshwa
kushtushwa na tukio hilo ambapo walikutwa wakitafakari nje ya hoteli
hiyo.
Uongozi wa hoteli hiyo
ulipotafutwa ili kutoa ufafanuzi juu ya tukio hilo uligoma kuzungumzia
kwa madai kwamba limefikishwa mbele ya vyombo vya usalama.
Muonekano wa nje ya hotel ya Lush Garden Business Hotel
Chumba alichofia marehemu namba 214
jamiiblog inawapa pole nyingi
familia ya marehemu pamoja na ndugu na jamaa kwa msiba huo
mkubwa,,,,Ndugu mdau wa blog hii tutaendelea kukuletea habari zaid juu
ya msiba huo
No comments:
Post a Comment