Mbunge
wa kuteuliwa, mh.James Mbatia, amegomea uteuzi uliofanywa na waziri
mkuu, Mizengo Pinda na kutaja sababu tatu za kukataa kushiriki katika
tume iliyoundwa kuchunguza matoke mabaya ya kidato cha nne ya mwaka
2012.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana,Mbatia alisema amegomea uteuzi huo kwasababu tatu.
Mosi ni kwamba hajapata barua rasimi ya uteuzi,lakini pia ana hoja
bungeni ambayo haijafika mwisho na tatu haiungi mkono tume hiyo.
Wakati huo huo,taarifa ya waziri mkuu alioitoa jana wakati akitangaza
wajumbe wa tume hiyo inaonyesha kuwa ufaulu umeshuka toka asilimia 89
mwaka 2005 mpaka ailimia 43 mwaka 2012.
Kwa maneno memgine, tangu Kikwete aingie madarakani ufaulu umeshuka toka asilimia 89 mpaka asilimia 43.
Source:Tanzania Daima online la tarehe 03/03/2013.

No comments:
Post a Comment