
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwasili katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro
usiku wa kuamkia jana Machi 15, 2013 akiongozana na Askofu wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude tayari kuhudhuria harambee ya ujenzi
wa kanisa jipya la Kigurunyembe. Zaidi ya Shilingi milioni 250 zilipatikana
katika harambee hiyo, ikiwa ni zaidi ya lengo la kupata milioni 200
walilojiwekea.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisimamia harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika
ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia
leo Machi 15, 2013. Kuume kwake ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro,
Mhashamu Telesphor Mkude.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe
iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku
wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akikabidhi kwa watawa keki maalumu iliyopigwa mnada na kununuliwa kwa zaidi ya
shilingi milioni moja. Aliitoa keki hiyo kama zawadi kwa watoto yatima
wanaolelewa na watawa hao.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete
na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude
wakipokea keki maalumu iliyopigwa mnada na kununuliwa kwa zaidi ya shilingi
milioni moja.
No comments:
Post a Comment