
Baadhi
ya Warembo walioshiriki Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 wakicheza
muziki wa aina ya Kwaito wakjati wa tafrija maalum ya uzinduzi wa
Mashindano ya Miss Tanzania 2013 Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Machi 14, 2013. Kulia ni Redd’s Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred.
Redd’s
Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred (katikati) akigonganisha glass na
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ni Wadhamini
wakuu wa Shindano la Miss Tanzania,Kushilla Thomas (klia) pamoja na
Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania,Anko
Hashim Lundenga ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka
Mrembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakati wa tafrija mchaparo a.k.a
mkia wa jogoo (cocktail party),iliyofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa
Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Lino International Agency ya Jijini Dar es Salaam, ambao
ndio waandaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akitoa
hotuba ya ufunguzi, wa Shindano la kumsaka Malkia wa Tanzania 2013.
Hii
ndio ilikuwa tatu bora ya Miss Tanzania 2012, Mshindi wa Taji la Redds
Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati) akiwa pamoja na washindi
wenzake, Eugene Fabian aliyetwaa nafasi ya pili (kulia) na Mshindi wa
Tatu, Edda Sylvester.
Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania, Mzee Ole Naiko (kulia) akizungumza na wanakamati ya Miss Tanzania na Miss Tanzania 2012.
Redds Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred akitoa hotuba ya ufunguzi, wa Shindano la kumsaka Malkia wa Tanzania 2013.
Banana Zoro na kundi zima la B Band lilitoa burudani.
No comments:
Post a Comment