ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Tuesday, March 19, 2013

Ziara Ya Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Mkoa wa Kaskazini Pemba


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akikata utepe kufungua madarasa mapya ya Skuli ya Msingi ya Ole,Jimbo la Ole Mkoa wa Kaskazini Pemba jana,akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa huo,(kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna,akizungumza na Walimu na wanafunzi wa Skuli ya msimgi Ole,Jimbo la Ole Mkoa wa Kaskazini Pemba jana,kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kuzungumza na wanafunzi na wananchi baada ya kufungua madarasa mapya skulini hapo. Picha na Ramadhan Othman Ikulu.
  Wanafunzi Jamila Abdalla Swaleh,(kushoto) na Haulat Yussuf Abdi,wakihani utenzi mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati wa Sherehe ya ufunguzi wa Madarasa mapya.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipokea risala wakati wa Sherehe ya ufunguzi wa Madarasa mapya.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wananchi wa Konde wilaya ya Wete, Pemba jana alipotembelea barabara ya Konde-Wete,inayojengwa na kampuni ya LEA Associates South AsiaPvt Ltd, chini ya ufadhili wa shirika la MCC la Marekani,akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Ole,Jimbo la Ole Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipozungumza nao baada ya kufungua madarasa mapya ya kusomea Skulini hapo jana.Picha na Ramadhan Othman Ikulu-Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...