Katika hali ya
kushitua,Mh.Mbowe akiongea na wanachama wa chadema jana Ubungo plaza
amemkaanga Zitto kabwe na kudai kuwa chadema haiko tayari kumtimua
Lwakatare katika chama hata kama ni gaidi....
"Eti nashangaa kuna watu wanataka
CHADEMA kimuache Lwakatare na kumsimamisha uongozi kwa uzushi
uliopandikizwa na CCM, Hilo halitafanyika"- alisema Mbowe.
Kuwajibika kisiasa ni pamoja na kuachia ngazi ya ukurugenzi wa usalama ili kupisha uchunguzi salama na kukiacha chama salama.
Katika barua yake kwa chama
chake,Zitto Kabwe alikitaka chama kijichunguze kuhusu shutuma hizi za
ugaidi zinazokikabili huku Lwakatare akiwa nje ya ulingo wa viongozi
waandamizi wa chadema.
Hata hivyo katika hali ya
kustaabisha barua ya zitto ilivuja na kusambaa mitandaoni wakati Zitto
Kabwe anadai kuwa ilikuwa ni barua ya siri kati yake na ofisi ya katibu
mkuu wa chadema....
Kauli ya Mbowe leo hii kumkana zitto Kbwe mbele ya wanachama wa inaleta sura mbili ndani ya chama hicho cha upinzani:
Mosi:Barua ya mapendekezo ya Zitto ilivujishwa kwa maksudi kama njia ya kumpinga zitto....
Pili: Kauli ya Mbowe ya leo
inamkingia kifua katibu mkuu kutowajibika kwa kuvujisha barua kwa sababu
barua haikubebe ujumbe wenye maana kwa chama na Lwaktare
Tatu: Madai ya UGAIDI dhidi ya
Lwakatare na Chadema kwa ujumla ni ya kweli ,hivyo chama kinajukumu la
kumlinda Lwakatare ili kuuficha ukweli usijulikana

No comments:
Post a Comment