ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, April 19, 2013

Makinda aweka ngumu wabunge waliofukuzwa bungeni kurudi kabla ya kipindi cha adhabu kwisha

Photo


Leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu Mh Spika ametoa uamuzi kuhusu muongozo ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano kwa wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa juzi na Naibu Spika. Mh Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu vjambo hilo uamuzi wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea tukio kama hilo.
Kwa uamuzi huo Wabunge hao watakosekana bunge bunge kwa siku tano ambazo ni Alhamisi (jana), Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na Jumatano wiki ijayo
Uamuzi wa Naibu Spika Mh. Job Ndugai, wa kumtoa nje Mh. Lissu, Mh. Sugu na wengineo, na kupewa adhabu ya kutoshiriki vikao vitano vya Bunge, Kutokana na Mh. Tindu Lisu Kuomba Muongozo/Taarifa mara kwa mara, Hivyo Kuingilia wengine katika kutoa hoja zao, na baadae kitendo cha wabunge hao kukaidi amri Halali ya Naibu Spika ya kutoka nje ya Bunge pamoja na kuwagomea Askari wabunge, kitendo ambacho kidogo kizue masumbwi live, Umebarikiwa na Mheshimiwa Spika kwa kufuata kanuni za Bunge, Hivyo Basi, Maamuzi ya Mh. Ndugai, yatakua Kanuni Rasmi kwa Tukio kama Hilo Na adhabu iliyotolewa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...