Mhe.Lowassa
MBUNGE
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ni miongoni mwa wabunge
watakaoshuhudia hafla ya waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa
kutunukiwa tuzo ya heshima leo mjini Iringa.
Akizungumza
kwa njia ya simu kutoka mjini Dodoma ,Filikunjombe alisema kuwa
anategemea kuwasili mjini Iringa kwa ziara ya siku moja kwa ajili
ya kumuunga mkono Lowassa katika mwaliko wake wa kushiriki harambee
ya kuchangia ujenzi wa Kanisa .
Mbunge Filikunjombe
Hata
hivyo waumini na uongozi wa huduma ya injili na uponyaji ya
Overcomers Power Center (OPC) chini ya Askofu Dkt Boaz Sollo ambao leo
wameandaa mapokezi makubwa kwake kwa ajili ya kumpokea Lowassa
kutoka katika uwanja wa Ndege Nduli majira ya saa 3 asubuhi
atakapowasili kwa Ndege na kuelekea katika ukumbi wa St Dominic
ambako kutafanyika shughuli hiyo kuanzia muda wa saa 6 mchana .
Akizungumza
na waandishi wa habari jana askofu Dkt Sollo alisema kuwa mbali ya
kumtunuku tuzo hiyo Bw Lowassa pia kiongozi huyo anataongoza
harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la kanisa la OPC linaloendelea
kujengwa katika eneo la zizi la Ng’ombe ambapo zaidi ya Tsh.
Milioni 250 zinahitajiika kukamilisha ujenzi wa jengo hilo pamoja na
kituo cha Radio Overcomers Fm (98.6 Mhz)kilichopo mjini Iringa .
Dkt
Sollo alisema kuwa lengo la OPC kumwalika na kumtunuku tuzo ya
heshima Bw Lowassa ni kutokana na kuwa jirani zaidi na jamii na
amekuwa akiitika wito wa makundi mbali mbali na kuyasaidia bila
ubaguzi wowote hivyo kutokana na mchango wake huo kwa jamii wao
kama kanisa wameona ni vema kuutambua mchango wake huo na kumwalika
ili kumpa tuzo hiyo maalum kama ahsante kwake.
“
Tuzo hiyo itampa moyo zaidi wa kuendelea kuwa karibu na jamii na
kutambua pia mapokeo ya jamii ambayo amekuwa akiisaidia mara kwa
mara….ikiwa ni pamoja na kuendelea kusaidia kuendeleza amani nchini
kwa kuchangia nyumba za ibada”
Askofu Dkt Sollo
Dkt
Sollo alisema kuwa Lowassa ambae ni mbunge wa jimbo la Monduli
mkoani Arusha amekuwa kipenzi cha wengi hata wale wasio wapiga kura
wake na kuwa uongozi wake kama waziri mkuu wengi walitokea
kumpenda na kuwa toka alipojiuzulu nafasi hiyo ya uwaziri mkuu
hajapata kufika mkoani Iringa hivyo sehemu kubwa ya wana Iringa wana
hamu kubwa ya kukutana nae kwa mara nyingine.
Hata
hivyo baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wamepongeza hatua
ya OPC chini ya Dkt Sollo kuamua kumtunuku tuzo hiyo Lowassa na kuwa
ni kweli anastahili kupewa tuzo kwani ni miongoni mwa viongozi
waadilifu na wachapa kazi hapa nchini.
No comments:
Post a Comment