ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Urais 2015. Show all posts
Showing posts with label Urais 2015. Show all posts

Saturday, June 15, 2013

Lowassa atangaza ndoto yake



Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwapungia mkono walimu walioshiriki katika hafla ya harambee ya kuchangia Saccos ya walimu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi, jana. 

  • Huku akimtaja Dk Martin Luther King aliyekuwa mwanaharakati wa haki za Wamarekani weusi aliyefariki kabla ya kuuona utimilifu wa ndoto yake, Lowassa alisema kuwa anamwomba Mungu asimwondoe duniani ili aweze kushiriki kuifanya ndoto hiyo kuwa kweli itakayokamilika siku si nyingi ambapo viongozi watakubali kuwa elimu bora ndiyo itakayowasaidia Watanzania kuchimba madini yao na kuyauza kwa faida duniani.


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema kuwa ana ndoto kwamba siku moja sekta ya elimu itapewa kipaumbele cha kwanza nchini na kuzikomboa rasilimali za taifa la Tanzania zinazowanufaisha wageni na kuacha wananchi wakiambulia faida kidogo.
Huku akimtaja Dk Martin Luther King aliyekuwa mwanaharakati wa haki za Wamarekani weusi aliyefariki kabla ya kuuona utimilifu wa ndoto yake, Lowassa alisema kuwa anamwomba Mungu asimwondoe duniani ili aweze kushiriki kuifanya ndoto hiyo kuwa kweli itakayokamilika siku si nyingi ambapo viongozi watakubali kuwa elimu bora ndiyo itakayowasaidia Watanzania kuchimba madini yao na kuyauza kwa faida duniani.
Akizungumza wakati wa kuchangia SACCOS ya walimu ya Moshi Vijijini, Ushirika wa Stadium jana, Lowassa alisema kuwa katika ndoto yake anawaona viongozi wakikubali kwamba elimu bora ndiyo italisaidia taifa kuumiliki utalii na kunufaika nao, badala ya kuwaachia wageni wanufaike nao, huku Watanzania tukiambulia makombo.
Wakati Lowassa akieleza ndoto yake hiyo, Mwenyekiti wa TLP na mbunge wa Vunjo Augustine Mrema amesema: “Biashara ya urais imenishinda namwachia Lowassa kwani mimi nimeamua kurudi kwenye biashara ya rejareja.”
“Ninayo ndoto kuwa siku si nyingi zijazo, elimu itapewa kipaumbele cha kwanza nchini Tanzania.
Na namwomba Mwenyezi Mungu asiniondoe duniani, kabla sijauona utimilifu wa ndoto hii kama Dk King (Martin Luther) alivyoondolewa kabla hajaiona ndoto yake ikitimia, bali namwomba anipe muda na nguvu, niweze kushiriki katika kuifanya ndoto hiyo iwe kweli,” alisema Lowassa.
Katika harambee hiyo ambapo zilipatikana jumla ya Sh1.3 bilioni , kati ya hizo fedha taslimu zilikuwa Sh250 milioni, Lowassa alifafanua kuwa itafika wakati ambapo elimu ya Tanzania itakuwa bora na kuwavutia majirani zake kuja kuwasomesha watoto wao nchini.
Akizungumzia kudorora kwa elimu nchini, Waziri Mkuu huyo wa zamani alisema kuwa bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya sekta ya elimu imekuwa ikitegemea fedha za wahisani kwa asilimia 70 na kwamba jambo la kusikitisha wahisani hao hawatoi fedha zote wanazoahidi, badala yake hutoa asilimia kati ya asilimia 40 na 50 ya fedha walizoahidi.
“Bajeti yetu ya maendeleo ya sekta ya elimu kila mwaka haitekelezeki kwa upungufu wa asilimia 30-35. Kwa hali hii tutapataje maendeleo katika sekta ya elimu?” alihoji Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli mkoani Arusha na kuongeza: “Mwaka 1992 tulikuwa na Watanzania asilimia 15 tu wasiojua kusoma na kuandika, ilihali hivi sasa tuna Watanzania takribani asilimia 31 wasiojua kusoma.”
Lowassa alisema kuwa wakaguzi wa shule za msingi na sekondari kushindwa kukagua shule zote nchini huchangia kushuka kwa elimu, akibainisha kwamba asilimia 20 pekee ya shule zote ndizo hukaguliwa kwa mwaka.
Alisema ili kufikia mafanikio yatakayoletwa na elimu, Serikali inapaswa kumjali mwalimu kwa kumpa motisha na mazingira mazuri ya kufundishia.
Akijibu hoja za watu wanaosema kuwa kuboresha huduma za walimu haiwezekani kutokana na idadi yao kuwa kubwa, alinukuu sehemu ya hotuba ya Rais wa zamani wa Marekani Franklin Roosevelt akisema: “ Kitu kimoja tunachopaswa kukiogopa ni woga wenyewe.”

Saturday, April 20, 2013

MBUNGE FILIKUNJOMBE KUSHUHUDIA TUZO YA LOWASSA IRINGA LEO, MAPOKEZI MAKUBWA YA KIFALME AANDALIWA

Mhe.Lowassa
MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ni miongoni mwa wabunge watakaoshuhudia hafla ya waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kutunukiwa tuzo ya heshima leo mjini Iringa.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mjini Dodoma ,Filikunjombe alisema kuwa anategemea kuwasili mjini Iringa kwa ziara ya siku moja kwa ajili ya kumuunga mkono Lowassa katika mwaliko wake wa kushiriki harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa .

Mbunge Filikunjombe
Hata hivyo waumini na uongozi wa huduma ya injili na uponyaji ya Overcomers Power Center (OPC) chini ya Askofu Dkt Boaz Sollo ambao leo
wameandaa mapokezi makubwa kwake kwa ajili ya kumpokea Lowassa kutoka katika uwanja wa Ndege Nduli majira ya saa 3 asubuhi atakapowasili kwa Ndege na kuelekea katika ukumbi wa St Dominic ambako kutafanyika shughuli hiyo kuanzia muda wa saa 6 mchana .

Akizungumza na waandishi wa habari jana askofu Dkt Sollo alisema kuwa mbali ya kumtunuku tuzo hiyo Bw Lowassa pia kiongozi huyo anataongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la kanisa la OPC linaloendelea kujengwa katika eneo la zizi la Ng’ombe ambapo zaidi ya Tsh. Milioni 250 zinahitajiika kukamilisha ujenzi wa jengo hilo pamoja na kituo cha Radio Overcomers Fm (98.6 Mhz)kilichopo mjini Iringa .
Dkt Sollo alisema kuwa lengo la OPC kumwalika na kumtunuku tuzo ya heshima Bw Lowassa ni kutokana na kuwa jirani zaidi na jamii na amekuwa akiitika wito wa makundi mbali mbali na kuyasaidia bila ubaguzi wowote hivyo kutokana na mchango wake huo kwa jamii wao kama kanisa wameona ni vema kuutambua mchango wake huo na kumwalika ili kumpa tuzo hiyo maalum kama ahsante kwake.
“ Tuzo hiyo itampa moyo zaidi wa kuendelea kuwa karibu na jamii na kutambua pia mapokeo ya jamii ambayo amekuwa akiisaidia mara kwa mara….ikiwa ni pamoja na kuendelea kusaidia kuendeleza amani nchini kwa kuchangia nyumba za ibada”
Askofu Dkt Sollo
Dkt Sollo alisema kuwa Lowassa ambae ni mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha amekuwa kipenzi cha wengi hata wale wasio wapiga kura wake na kuwa uongozi wake kama waziri mkuu wengi walitokea kumpenda na kuwa toka alipojiuzulu nafasi hiyo ya uwaziri mkuu hajapata kufika mkoani Iringa hivyo sehemu kubwa ya wana Iringa wana hamu kubwa ya kukutana nae kwa mara nyingine.
Hata hivyo baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wamepongeza hatua ya OPC chini ya Dkt Sollo kuamua kumtunuku tuzo hiyo Lowassa na kuwa ni kweli anastahili kupewa tuzo kwani ni miongoni mwa viongozi waadilifu na wachapa kazi hapa nchini.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...