Dar es Salaam. Polisi katika Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, wamekamata magari manne ya wizi likiwamo moja lililoibwa
kutoka nchini Msumbuji.
Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova
alisema magari hayo yamekamatwa katika operesheni ya polisi iliyodumu
kwa siku mbili.
Kova pia alisema mbali na kukamata magari hayo, polisi pia wamekamata silaha nane zikiwamo bunduki sita na bastola mbili.
Kova pia alisema mbali na kukamata magari hayo, polisi pia wamekamata silaha nane zikiwamo bunduki sita na bastola mbili.
Pia risasi 27 zilizokuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya uhalifu.
Alisema magari yaliyokamatwa ni pamoja Ford Ranger, gari ambalo liliibwa Msumbiji. Mengine ni Mitsubish Canter, Toyota Noah na Toyota Cresta.
Alisema magari yaliyokamatwa ni pamoja Ford Ranger, gari ambalo liliibwa Msumbiji. Mengine ni Mitsubish Canter, Toyota Noah na Toyota Cresta.
Kwa mujibu wa kamanda, watuhumiwa watano
wamekamatwa wakihusishwa na wizi huo na watafikishwa mahakamani baada ya
kukamilika kwa uchunguzi
Katika operesheni hiyo iliyohusisha mikoa yote
mitatu ya kanda maalumu, ambayo ni Ilala, Kinondoni na Temeke daladala
447 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani.
Kamanda Kova alisema jumla ya Sh26.5 milioni zilikusanywa kutokana na faini za makosa hayo.
Kamanda Kova alisema jumla ya Sh26.5 milioni zilikusanywa kutokana na faini za makosa hayo.
Naye Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles
Kenyela amesema jeshi hilo mkoani kwake linaendelea na operesheni ya
kuwasaka wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba.
Alisema hadi juzi walikuwa wanawashikilia wanawake
wanane waliowakamata katika eneo la Uwanja wa Fisi, Tandale,
wakijihusisha na biashara hiyo.
Tatizo la baadhi ya wanawake kujihusisha na biashara ya kuuza miili yao, imekithiri zaidi katika mitaa ya katikati jijini.
Tatizo la baadhi ya wanawake kujihusisha na biashara ya kuuza miili yao, imekithiri zaidi katika mitaa ya katikati jijini.
Mara kadhaa wanawake wa aina hiyo wamekamatwa na
kufikishwa mahakamani, lakini hatua hiyo haijasaidia sana katika
kukomesha biashara hiyo.
Baadhi ya wanawake waliowahi kuhojiwa kuhusu kiini
kinachowasukuma kuuza miili yao bila hata kujali kuambukizwa virusi vya
ugonjwa wa Ukimwi, wamedai kuwa hali ngumu ya maisha ndiyo
inayowasukuma.
Walisema wanafanya hivyo, ili kupata fedha za kuwawezesha kujikimu kimaisha. Baadhi yao wamekiri kutokutumia mipira.
No comments:
Post a Comment