Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Silvacius
Likwelile pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr.
Philip Mpango akiwasilisha mpango wa maboresho katika Elimu, Maji,
Nishati, Usafirishaji, Rasilimali Fedha na Kilimo.
Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Dr.Mpango akijibu hoja
mara baada ya kuwasilisha mpango wa maboresho. Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha Dr. Silvacius Likwelile na Kaimu Balozi Ubalozi wa Tanzania Washington DC Bibi Lily Munanka.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia katikati akifafanua jambo wakati wa
majadiliano, kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania,
Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi
Bw. Philippe Dongier akifafanua jambo katika majadiliano hayo.
Ujumbe kutoka Benki ya Dunia wakifuatilia kwa makini wakati Dr. Mpango akiwasilisha mpango wa maboresho hayo
Ujumbe wa Tanzania ukuiwasilisha mpango wa maboresho ya maendeleo kwa Benki ya Dunia. Mpango huo unahusu maendeo katika maeneo ya Elimu, Maji, Nishati, Rasilimali Fedha, Kilimo na Usafirishaji.Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi. Eva Valerian – Washington DC
---
Ujumbe wa Tanzania uliohudhuria mikutano ya majira
ya kipupwe mjini Washington DC wapata fursa ya kufanya majadiliano na
timu nzima ya Benki ya Dunia kuhusu namna ya kuleta maendelea ya haraka.
Majadiliano haya yaliwasilishwa na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume
ya Mipango Dr. Philip Mpango ambaye aliwasilisha vyema mkakati mpya
wa Big Results Now.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Silvacius
Likwelile alisema kuwa fursa waliyoipata imewawezesha kuelezea mpango
huu mpya ambao utatuletea matokeo makubwa na ya haraka hivyo walimwomba,
Dr. Mpango aelezee msukumo mzima wa mpango huo.
Katika kuwasilisha mpango huo, Dr. Mpango alisema
kuwa mfumo huu mpya ambao Serikali yetu imeamua kuufanya utaboresha
upya utendaji kazi ndani ya Serikali. ”Tumeamua kuanza na maeneo muhimu
sita ambayo ni kilimo, usafirishaji, nishati, maji, elimu na rasilimali
fedha.” Alisisitiza Mpango.
“Kwa upande wa usafirishaji serikali itahakikisha
bandari ya Dar es Salaam, reli ya kati pamoja na barabara za ukanda
wa kati zinafanya kazi kwa ufanisi zaidi”. Aliongeza Mpango. Akizungumzia
nishati alifafanua kuwa lengo kubwa la serikali ni kuhakikisha kwamba
tatizo la umeme linatatuliwa kwa haraka ili kuweza kuchochea ukuaji
wa uchumi wenye kasi zaidi. Kwa upande wa suala la maji nalo halikuachwa
nyuma kwani kwa sasa maji ni kilio kikubwa kwa wananchi wetu walioko
vijijini .Alisema Mpango.
“Kwa upande wa Elimu Serikali imedhamiria kupitia
utaratibu huu wa matokeo makubwa sasa ili ilete mabadiliko ya haraka
kutoka asilimia 41 nakufikia asilimia 60 kwa mwaka 2013 na hatimaye
kufikia asilimia 80 ya kiwango cha ufaulu kwa miaka mitatu ijayo yaani
kufikia mwaka 2015. Eneo la rasilimali fedha ambazo zitaweza kusaidia
katika maeneo haya tuliwaeleza mbinu ambazo zitaibua vyanzo vipya vya
mapato ya kodi na yasiyo ya kodi lakini pia namna bora zaidi yakutumia
sekta binafsi ili kusaidia Serikali” Alisema Mpango.
“Jambo la kujivunia katika hili ni kwamba utaratibu
huu ni wa kwetu wenyewe na serikali ndio imebuni na kuanza kuutekeleza
sisi wenyewe, sio jambo ambalo tumesukumwa na wafadhili, bali viongozi
wetu wameusimamia ili uweze kufanikiwa na hatimaye wananchi waweze kupata
maisha bora zaidi.” Alisema Mpango.
Benki ya Dunia kwa kuona umuhimu wa mpango huu wameonyesha
maeneo ambayo serikali itashirikiana nao ili kuhakikisha kwamba mfumo
huu unafanikiwa.
Kwa kuhitimisha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
Dr. S. Likwelile alisema kuwa “Benki ya Dunia imeunga mkono jitihada
hizi na kwamba rasilimali chache tulizonazo zitatuwezesha kuzaa matunda
na kwamba watafanya kazi pamoja na serikali ya Tanzania kuhakikisha
kwamba mipango yote tunayofanya ielekezwe katika kuzaa matunda katika
Elimu, Nishati, Usafirishaji, Kilimo, Maji na Rasilimali Fedha. Na kikubwa
walichosisitiza ni suala la uwazi na namna gani raia wa kawaida anaweza
kushirikishwa katika kutoa maoni yao.
Imetolewa na Msemaji – Wizara
ya Fedha
Bi. Ingiahedi Mduma
Washington DC
19/04/2013
No comments:
Post a Comment