ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, April 22, 2013

Taswira Kutoka Mwanza Za Mkutano Mkubwa Wa Hadhara Uliyofanywa na Wabunge Wa Chadema Waliyosimamishwa Kuria Vikao Vitano vya Bunge na Naibu Spika Job Ndugai


Mbunge wa Ilemela-Chadema  Highness Kiwia akiunguruma mbele ya Maelfu ya Wanachama wa Chadema Mkoani Mwanza
Mbunge wa Iringa-Mjini-Chadema Mchungaji Peter Msigwa
Sehemu ya Maelfu ya Wanachama wa Chadema Mkoani Mwanza Wakiwasikiliza Mbunge wa Iringa-Mjini-Chadema Mchungaji Peter Msigwa na  Mbunge wa Ilemela-Chadema  Highness Kiwiawalipokua wakihutubia mkutano wa Hadhara Mwanza Jana.Picha na Chadema
 -- 
 Wabunge sita wa Chadema waliosimamishwa bungeni wameamua kwenda kuwashtaki Spika Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai kwenye majimbo yao.

Wakitangaza uamuzi huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi ya Mbugani, Mwanza jana, walisema pia watakwenda kwenye majimbo ya wabunge wawili wa CCM, Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Livingstone Lusinde (Mtera) ili kueleza jinsi wabunge wa upinzani wanavyokandamizwa bungeni.
Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa (CCM), aliwasimamisha wabunge sita wa Chadema kuhudhuria vikao vitano vya Bunge kutokana na kile alichokiita kufanya vurugu bungeni. Hatua hiyo ya Ndugai aliyoichukua Aprili 17, mwaka huu ilipata baraka za Spika Makinda Ijumaa iliyopita.

Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Ezekiah Wenje (Nyamagana). Katika mkutano huo ulioanza saa 9.30 alasiri na kumalizika saa 12.00 jioni, ulihudhuriwa na wabunge wanne kati ya hao. Mbilinyi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhutubia akifuatiwa Mchungaji Msigwa, Kiwia na Wenje. Lissu na Lema hawakuhudhuria.

Akizungumzia ziara yao katika majimbo ya viongozi hao wa Bunge, Mchungaji Msigwa alisema itakuwa ya kuwashtaki kwa kuendesha Bunge kuwapendelea wabunge wa CCM hata wanapofanya makosa ya waz

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...