
(PICHA NA PHILEMON SOLOMONWA FULLSHANGWE )
********
SERIKALI
inasikitishwa na baadhi ya Asasi za kirai na vyombo vya habari
vinavyopotosha ukweli kuhusu mgogoro wa ardhi katika eneo la Pori
Tengefu la Loliondo.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Kagasheki
amesema kuwa eneo la pori tengefu la Loliondo ni miliki halali ya
serikali kwa mujibu wa sheria ya umilikaji ardhi tokea kabla na baada ya
ukoloni.Historia inaonyesha kuwa mwaka 1902 utawala wa ujerumani
walitunga sheria ya umiliki na matumizi ya ardhi ambapo ardhi ilibaki
kuwa chini ya serikali,vivyo hivyo kwa utawala wa Waingereza mnamo mwaka
1923 na 1974 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu mgogoro huo Kagasheki amesema kuwa kinachofanyika sasa
ni Serikali kumega ardhi yake na kuwapatia wananchi na si kama
inavyoripotiwa na vyombo vingi vya habari.
No comments:
Post a Comment