DAVID BECKHAM alitoka Uwanjani
katika Mechi yake ya mwisho ya Nyumbani ya Klabu yake Paris St-Germain
ambayo huenda ikawa ndio ya mwisho katika maisha yake ya Soka ya Miaka
20 huku akibubujikwa machozi.
Beckham, ambae alianza Mechi hiyo ya
Ligi dhidi ya Brest kama Nahodha, alibadilishwa katika Dakika ya 81 na
Mechi kusimama kwa muda huku Wachezaji wenzake wa PSG wakimshangilia na
yeye akawa akitoka nje kwa machozi.
Mashabiki wengi wa PSG wamekuwa wakililia Beckham, Miaka 38, abakie kama Mchezaji badala ya kustaafu.
Msimu huu PSG ndio wamekuwa Mabingwa
wa France na bado wana Mechi moja ya Ligi Jumapili ijayo watakayocheza
Ugenini na Lorient lakini inaaminika Beckham hatakuwepo.
Katika Mechi ya Jana PSG waliifunga
Brest Bao 3-1 huku Beckham akitengeneza Bao moja kwa Kona yake
kuunganishwa na Blaise Matuidi na Bao nyingine mbili kufungwa na Zlatan
Ibrahimovic.
Bao la Brest lilifungwa na Charlison Benschop.
Mara baada ya Filimbi ya mwisho
kwenye Mechi hiyo na Brest, Beckham aliwahutubia Mashabiki na kusema:
“Nataka kumshukuru kila Mtu hapa Paris-Wachezaji wenzangu, Wafanyakazi
na Mashabiki. Ni kitu kikubwa kumalizia Soka langu hapa. Nimemaliza Soka
nikiwa Bingwa na kwenye Timu iliyonifanya nijione kama nimekaa Miaka
10!”
Wachezaji wa PSG walimbeba na
kumrusharusha juu huku akishuhudia na Mkewe Victoria na Rais wa zamani
wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.

SIFA KUBWA: David Beckham aliungana na watoto wake kushangilia ubingwa ligi ya Ufaransa ambapo amewasaidia PSG kutwaa ndoo hiyo.

Baada ya kipenga cha mwisho, wachezaji wa PSG walikuwa wanamrusha Beckham juu

Baada ya kutolewa uwanjani hapo jana, Beckham alionekana akiwa hivyo


MACHOZI YAKIMTOKA: David Beckham alitokwa na machozi baada ya kuona
kocha wake Carlo Ancelotti anataka kumtoa uwanjani ili kumpisha mchezaji
mwingine

Wachezaji wa PSG wakimkumbatia Beckham baada ya kufanyiwa mabadiliko

No comments:
Post a Comment