KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
 (CCM) Abdulrahman Kinana amesisitiza kwamba Chama kitamwadhibu bila 
huruma mwanachama yeyote anayejipitisha-pitisha katika maeneo mbalimbali
 na kufanya kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.
Kinana alisema hayo leo wakati 
akizungumza na Kamati ya Siasa na mkoa wa Iringa, katika kikao maalum, 
kilichofanyika kabla  ya kwenda mkoani Njombe ambako ameanza ziara ya 
siku saba mkoani humo.
Kinana alisema, katazo la 
wanachama kujipitisha-pitisha na kupiga kampeni za kuwania urais au 
nafasi yoyote kabla ya muda  halitoki midomoni mwa viongozi bali ni kwa 
mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.
“Ndugu zanguni, nawakumbusha 
kwamba kwa hili hatuna mzaha nalo, hivyo hakikisheni kila mmoja wenu 
kama kiongozi hajihusishi kwa namna yoyote kushiriki katika kutumiwa na 
wanachama hao wanaojipitishajiptisha”, alisema Kinana na kuongeza;
“Ni lazima Chama kiwe kikali 
kwenye jambo hili, kwa sababu kama kitawaacha watu hawa kukiuka taratibu
 na kanunzi za Chama wanazidi kukifanya chama kuwa na makundi mengi 
ambayo yatakipeleka pabaya,” alisema Kinana
Kinana alisema,  kazi walioyonayo 
wale wote wanaokitakia mema Chama, ni kumuunga mkono Mwenyekiti, Rais 
Jakaya katika kazi ya kuhakikisha CCM inakamilisha utekelezaji ilani 
yake ya Uchaguzi kwa kiwango kinachostahili na siyo muda kujipitisha 
pitisha mtu binaafsi kwa wanachama huku utekelezaji wa ilani ukisinzia.
Alisema kuwa hivi sasa kazi ya CCM
 ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya uchaguzi kwa kipindi kilichobaki 
cha miaka miwili ya nusu kabla ya kumalizi kwa awamu ya uongozi wa Rais 
Jakaya Kikwete.
“Ni wazi kazi yatu CCM ni 
kuhakikisha tunatekeleza ilani ya uchaguzi kwa vitendo na si mamneno 
kama wanavyofanya wengine. ni kazi kubwa imefanyika chini ya uongozi wa 
Rais Kikwete na katika kipindi cha miaka miwili iliyobaki tumedhamiria 
kuifanya zaidi”, 
Alisema moja ya maeneo ambayo 
licha ya kuwepo changamoto za hapa na pele lakini yamefanikisha sana 
utekelezaji wa ilani ya CCM,  ni kwenye Halmashauri mbalimbali nchini 
ambapo watendaji walio wengi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutekeleza
 miradi ya maendeleo kwa kasi.
“Kwa kweli CCM lazima hawa 
tuwapongeze maana kuna wengine kazi yao imebaki kuwashambulia huku 
wakijua watendaji hao hawana fursa ya kujitete mbele ya jamii. chapeni 
kazi nasi tupo nyuma yenu, na kila wakati tutakuwa tukitambua juhudi na 
kazi kubwa mnayoifanya kwa jamii,” alisema Kinana.
 
 
 
 
 
 

 
 

No comments:
Post a Comment