Hawa ndiyo washirikiwa Bigi Brother Africa 2013. "The Chase" Mtandao wako wa kijamii wa Goldentz unakuletea majina ya washiriki na nchi wanazotoka. Mtanange huu wa miezi mitatu utakuwezesha wewe mtazamaji kupata uhondo wa aina yake pale washiriki 28 ambao wanaishi sehemu moja bila kujali jinsia zao, wakishindania bingo la dola za kimarekani 300,000. Mtanange huo utahusisha namna wanavyoweza kuishi kwa pamoja, kushirikiana lakini zaidi ni namna watu ambao wanajua kuna kamera kila kona na microphone wanavyoweza kuishi bila kuigiza. Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, wengine watajikuta wanaanzisha uhusiano wa kimapenzi, wengine kugombana, wengine kufitiniana, wengine kutoana..... Wewe na mimi tutapaswa kupiga kura kumwokoa Mtanzania atakayeingia katika denja zoni na kupiga kura ya kumwondoa wa nchi nyingine ambaye wewe utaona kama ni kikwazo kwa Mtanzania. Wapiga kura ndiyo wanaowaokoa mamates wa big brother. Ni matumaini yangu kuwa kama siyo Nando basi atakuwa Feza ambaye ataibuka mshindi wa milioni za Kitanzania 4480,000,000/=



Who are you rooting for? Big Brother Africa The Chase! It’s on.
No comments:
Post a Comment