ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Sunday, May 5, 2013

Picha na maelezo mbalimbali ya milipuko ya mabomu katika kanisa Katoliki Arusha

WATU WAKIWA WAMEZIRAHI BAADA YA MLIPUKO WA BOMU KUTOKEA ENEO HILO
DSC_0280Majeruhi wakihangaika huku na kule mara baada ya kutokea kwa mlipuko katika kanisa la Katoliki jijini Arusha
 Hii ni njia ya kuelekea olasiti kanisani ambapo mlipuko mkubwa umetokea leo asubuhi wakati wa misa ya ufunguzi wa kigango ambapo mgeni rasmi alikuwa ni balozi wa papa nnchini tanzania
Umati wa  wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo.
 Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja  amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.
 Waumini  pamoja na baadhi ya wanacchi wakiwa katika hali ya taharuki  wasiamini nini kilichotokea  kutokana na mlipuko mkubwa  uliotokea asubuhi ya leo.


 Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia  leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka.
Polisi waki imarisha doria eneo la tukio   baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali kupatiwa matibabu zaidi ...Mpaka tunaondoka eneo la tukio Viongozi mbali mbali akiwemo mmbunge wa arusha walikuwemo eneo hilo.


Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya..


Mungu uwe upande wetu
Majeruhi wa Mlipuko huo akipata huduma ya kwanza mapama baada ya tukio hilo
eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu ndipo kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu ndipo kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....

Makamu wa raisi Dkt Mohamed Gharib Bilal Pamoja na Stephen Masele wakiwapa pole majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea majira ya saa 4;35 asubuhi jana kwenye uzinduzi wa kanisa la st.Joseph Mfanyakzi maeneo ya Olasit jijini Arusha.
 Makamu wa raisi Dkt Mohamed Gharib Bilal Pamoja na Stephen Masele wakiwapa pole majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea majira ya saa 4;35 asubuhi jana kwenye uzinduzi wa kanisa la st.Joseph Mfanyakzi maeneo ya Olasit jijini Arusha.
 Makamu wa raisi Dkt Mohamed Gharib Bilal Pamoja na Mh.Stephen Masele wakiwapa pole majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea majira ya saa 4;35 asubuhi jana kwenye uzinduzi wa kanisa la St.Joseph Mfanyakzi maeneo ya Olasit jijini Arusha
Makamu wa raisi Dkt Mohamed Gharib Bilal Pamoja na Stephen Masele wakiwapa pole majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea majira ya saa 4;35 asubuhi jana kwenye uzinduzi wa kanisa la st.Joseph Mfanyakzi maeneo ya Olasit jijini Arusha.
Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT)Dkt Alex Malasusa akiwafariji wananchi baada ya kupewa nafasi ya kuwaombea majeruhi waliolazwa katika hospital ya Mount meru jijini arusha jana baada ya kulipukiwa na kitu kinachodhani kuwa ni bomu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha.  Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa.  

Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake. 

Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.  Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali na vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili.  
 
"Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma.  Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine, uwe na chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi yetu.  
 
"Kamwe hatutakubali kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake" amesema Rais ambaye anaamini kuwa Serikali, kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu hao watapatikana na kuadabishwa ipasavyo.
 
 Aidha, Rais Kikwete anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wafiwa na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo. Anaungana nao katika machungu na msiba. Rais pia anawaombea wote walioumia katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa.

Rais Kikwete vilevile anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na shughuli yao muhimu ya uzinduzi wa Kanisa lao.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
 5 Mei, 2013

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...