Papa Francis akibariki waumini kwa Ekaristi Takatifu
Wakristo wakibeba hema lililofunika Padre aliyebeba Monstrance yenye Ekaristi Takatifu.
panis triticeus et vinum de vite (ngano na mzabibu) ambavyo ndivyo elements vinavyotumika katika kugeuzwa kuwa Mwili na Damu ya Yesu
Huu
ndio mwili wangu; hii ndiyo damu yangu. Jumapili hii tunaadhimisha Siku
kuu ya Mwili na Damu ya Kristo. Siku kuu yeneyewe yatusaidia kutafakari
juu ya umoja uliopo baina yetu na Kristo, kwani sisi tu viongo vya
mwili wake. Kwenye Mkutano Mkuu wa Sinodi ya Maasikofu wa Afrika, Sinodi
ilisema, "Kanisa bara letu Afrika tu Jamaa ya Mungu". Twajua kwamba
pakiwa na umoja kwenye familia, pia kuna ushirikiano. Hivyo pia, viungo
vya mwili vikiwa na ushirikiano, mwili mzima hupata nguvu, utulivu na
furaha. Lengo la siku kuu hii hasa ni kuonyesha umoja wetu na furaha
yetu katika Kristo, anayetupatia mwili wake na damu yake, kama chakula
cha uzima. Kwenye Somo la kwanza twasikia jinsi Mungu alivyofanya agano
lake na wana wa Israeli. Mungu aliwapa amri za wokovu, na Waisraeli
walihahidi kuzitimiza kwa kudhihirisha agano hilo kwa damu ya wanyama.
Somo la pili yatuonyesha jinsi Mungu alikamilisha agano lake na kuilitia
muhuri kwa damu ya Mwanae ili kutakasa roho zetu. “Kwa damu ya Kristo,
mambo makuu zaidi hufanyika!”. Injili ya siku kuu hii yatuonyesha Yesu
akifanya mujiza wa kuzidisha mikate 5 na samaki 2, ili umati wa watu
wale. Tunasikia kwamba wote walikula na wakashiba. Lengo hasa ya kula
pamoja ni kutuonyesha jinsi Mungu uwashibisha waku wake wote bila
kubagua. Hivyo pia ndiyo ishara kubwa la Sakramenti kuu ya Ekaristi.
Hivyo
sherehe za Ekaristi katika Misa takatifu ni kiini cha umoja wetu na
Kristo unaofikia kilele chake wakati wa Komunio Takatifu. Lakini
ijapokuwa Ekaristi yatulisha ki-roho, huenda tukasahahu jinsi Ekaristi
inao upande wa kuzingatia haki za ki-binadamu. Sherehe za Mwili na Damu
ya Kristo ndio wakati unaofaa wa kutafakati na kutia maanani jinsi
Ekaristi inahusiana na haki. Wakati wa Mwaka wa Jubileo ya Ekaristo
Oktoba 2004 hadi Oktoba 2005, Baba Mtakatifu, Yohane Paulo II kwenye
Barua yake Mane Nobiscum Domine (Bwana Kaa Nasi) alisema: “Si tungefanya
Mwaka huu wa Ekaristi wakati ambao kila Jimbo na kila Parokia
kujiazimia kwa njia ya pekee kujihusu na mojawapo ya aina za umasikini
duniani? Baba Mtakatifu alionya kwamba “Kigezo kitakaothibitisha sherehe
zetu za Ekaristia Takatifu kitakuwa upendo wetu kwa wenzetu na hasa
kujishugulisha na wale wasiojiweza.” Mtakatifu Paulo amesema kwamba
Jumuiya ya Kikristo “haifai” kusherekea Karamu ya Bwana baina ya
ugawanyifu na kutowajali masikini (1 Kor. 11:17-22, 27-34). Katekisimu
ya Kanisa Katoliki yatuambia: “Kupokea kwa ukweli Mwili na Damu ya
Kristo aliyotutolea, yatulazimu kumgudua Kristo katika masikini wa
mwisho, ndugu yake.” (Na. 1397). Sherehe ya Mwili na Damu ya Kristo
hukumbukwa hasa kwa sababu ya maandamano ya kuvutia ya Ekaristi.
Maandamano hayo pia ni wito kwetu ili kama Kristo nasi pia tuwe tayari
kumwaga damu yetu kwa ajili ya wengine. Wakati wa ubaguzi wa rangi huko
Namibia, Kanisa Katoliki ilitumia maandamano ya Siku kuu hii, kama
ishara ya kuwepo kwa Kristo baina ya watu, wakati wanaotetea haki zao.
Ekaristi basi ilikuwa ukumbusho wa kweli wa kujitoa kwa Kristo msalabani
ili kuondoa nyororo za dhambi na ukatili. Kuna ujumbe gani tungepeleka
nyumbani? 1) Ekaristi ni ukumbusho wa kweli kuhusu sadaka aliyotoa
Kristo ili kutukomboa sisi zote kutoka chochote kinachowakatili
binadamu, hasa sana kutokana na dhambi. 2) Hivyo, ndio sababu sherehe za
Mwili na Damu ya Kristo katika nchi za kiukatili zatoa ushuhuda mkali
na kuudhiwa na serikali dhalimu kama kule Namibia wakati wa ubaguzi wa
rangi. 3) Sherehe za Mwili na Damu ya Kristo haziwezi kutenganishwa na
udhalimu uliopo kwenye jumuiya yetu, kwa sababu uadhimisho wa Ekaristi
ni utangazaji wa haki za wanaodhalimiwa. 4) Basi Siku kuu ya leo
itathibitishwa uaminifu wetu ikiwa tutawakumbuka hasa wale wasio na
chakula na cha kunywa, yaani wote ndugu na dada za Bwana wetu Yesu
Kristo.
©2013 John S. Mbinda
No comments:
Post a Comment